Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la Maua kwenye kaburi la Linah George Mwakyembe, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mazishi yaliyofanyika leo Kyela Mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Linah George Mwakyembe, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe katika mazishi yaliyofanyika leo Kyela Mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimfariji Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha Mke wake Linah George Mwakyembe. Mazishi walifanyika leo huko Kyela Mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harisson Mwakyembe pamoja na familia yake wakiwa pamoja na waombolezaji wakati wa Ibada ya ya mazishi ya mkewe, Linah George Mwakyembe yaliyofanyika leo Kyela Mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kushiriki katika mazishi ya mke wa Waziri huyo, Linah George Mwakyembe yaliyofanyika leo Kyela Mkoani Mbeya. Kulia ni mkewe Mary (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)