Waziri Mkuu Aongoza Waombolezaji Kuaga Miili ya Waliofariki Katika Ajali ya Ndege ya Shirika la Precision
Nov 07, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji waliojitokeza kuaga miili ya watu waliopata ajali katika ndege ya Shirika la Precision, iliyotokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salamu za mwisho kwa miili ya watu waliopata ajali ya ndege ya Shirika la Precision iliyotokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa pole kwa ndugu wa Marehemu waliojitokeza katika uwanja wa Kaitaba yalipofanyika maombolezo ya kitaifa ya wahanga wa ajali ya ndege ya Shirika la Precision, ajali hiyo ilitokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba - Bukoba mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza na kumfariji kijana, Jackson Majaliwa kwa ushujaa wake wa kuwahi katika eneo ilipotokea ajali ya ndege ya Shirika la Precision na kuwaokoa abiria waliokuwa wameshindwa kutoka ndani ya ndege hiyo. Maombolezo ya kuaga miili ya watu wa ajali hiyo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera 7/11/2022.
Miili ya marehemu waliofariki katika ajali ya ndege ya Shirika la Precision iliyotokea Novemba 6, 2022, ikiwa imewekwa katika eneo maalum kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu katika maombolezo yaliyofanyika kweye uwanja huo Jumatatu 7/11/2022.
Ndege ya Shirika la Precision iliyopata ajali Novemba 6, 2022 ikiwa pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuvutwa kutoka eneo la ajali.