Waziri Mkuu Aongoza Mbio za NMB za Kuchangia Fedha Matibabu ya Fistula
Oct 01, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa medali ya kumaliza mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon) na Mwenyekiti wa Benki hiyo, Dkt. Edwin Mhende baada ya kumaliza mbio hizo zilizoanzia Viwanja vya Leaders Club na jijijini Dar es salaam, Oktoba 01, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kumaliza kilomita 5 za mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon) za kuchangia matibabu ya wanawake wenye tatizo la Fistula. Mbio hizo zilianzia katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, na kuishia katika viwanja hivyo, Oktoba 01, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 600 kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna kwa ajili ya kuchangia matibabu ya wanawake wenye tatizo la Fistula, baada ya kumaliza mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon) zilizoanzia katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, na kuishia katika viwanja hivyo, Oktoba 01, 2022. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhende
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi milioni 600 Afisa Mtendaji Mkuu wa CCRBT, Brenda Msangi kwa ajili ya kuchangia matibabu ya wanawake wenye tatizo la Fistula, baada ya kumaliza mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon) zilizoanzia katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, na kuishia katika viwanja hivyo, Oktoba 01, 2022. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna na Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhende.