Waziri Mkuu Akutana na Uongozi wa Jiji la Dar Es Salaam
Aug 18, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa jiji la Dar es Salaam katika kikao cha pamoja kujadiliana namna ya kuboresha utalii wa fukwe kwa lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii. kikao ambacho kilijadili namna bora ya kutumia maeneo ya wazi ya jiji hilo. Agosti 17, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Katika kikao cha pamoja cha kujadiliana namna ya kuboresha utalii wa fukwe kwa lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii jijini Dar es Salaam, Agosti 17, 2021.