Waziri Mkuu Afungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia
Jul 19, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watendaji wa Wizara ya Elimu na Tume ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU), baada ya kufungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam . Julai 19, 2022. Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Charles Kihampa, Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Penina Muhando na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Profesa James Mdoe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ndege isiyokua na rubani inayotumika kupiga picha za anga kwa ajili ya kuandaa ramani za msingi zinazowezesha kupanga miji, wakati alipofungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam . Julai 19, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia kompyuta mpakato inayotumia mwanafunzi ya Chuo Kikuu Huria, mwenye uono hafifu, Bernadeta Msigwa kwa kuandikia vitabu, wakati alipofungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam . Julai 19, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ngao ya shukrani kwa kufungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Julai 19, 2022. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Charles Kihampa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria katika ufunguzi wa Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam . Julai 19, 2022