Waziri Mkuu Afanya Ziara ya Siku Mbili Mkoani Singida
Aug 05, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Iglanson, kilichopo katika Wilaya ya Ikungi, akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Singida. Agosti 5, 2022. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi.
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Iglanson, kilichopo katika Wilaya ya Ikungi. Agosti 5, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa ramani baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Ikungi, akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Singida. Agosti 5, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Ikungi, akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Singida. Agosti 5, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Singida Agosti 5, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Singida. Agosti 5, 2022