Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mchengerwa Ahudhuria Mashindano ya Ligi ya UEFA EUROPA
Oct 07, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa jana Oktoba 6, 2022 amehudhuria mashindano ya ligi ya UEFA EUROPA kwa mualiko maalum kutoka kwa Rais wa Klabu ya Fenerbahce Ali Koc.

Waziri Mchengerwa alipata wasaa wa kushuhudia mechi kati ya Fenerbahce na AEK Larnaca, mechi iliyochezwa katika uwanja wa klabu hiyo nchini Uturuki.

Katika mechi hiyo timu ya Fenerbahce wameibuka washindi dhidi ya AEK kwa goli 1-0.

Akizungumza mara baada ya mechi, Rais huyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kuinua sekta ya michezo nchini.

Waziri Mchengerwa aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Lt. Gen. Yacoub Mohamed.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi