Waziri Masauni Akutana na Kufanya Mazungumzo na Kamishna Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi, Jijini Geneva nchini Uswisi
Oct 12, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (Wapili kulia) akimsikiliza Msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Gillian Triggs, akizungumzia masuala ya Wakimbizi katika ukumbi mdogo wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa wakati wa Kikao cha 73 cha Kamati Tendaji ya Shirika hilo jijini Geneva, nchini Uswisi, leo. Kulia ni Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania nchini Uswisi, Maimuna Tarishi na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (Wa pili kulia) akizungumza na Msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Gillian Triggs kuhusu masuala ya Wakimbizi katika ukumbi mdogo wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa wakati wa Kikao cha 73 cha Kamati Tendaji ya Shirika hilo jijini Geneva nchini Uswisi, leo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akifurahia jambo na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, nchini Uswisi, Maimuna Tarishi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi wakati alipokuwa anatoka kuzungumza na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi katika Kikao cha 73 cha Kamati Tendaji ya Shirika hilo jijini Geneva, nchini Uswisi, leo Oktoba 12, 2022.