Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Kalemani Akagua Umeme Nyumba kwa Nyumba
Jun 29, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53651" align="aligncenter" width="720"] Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isamilo, Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, akiwa katika ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini, Juni 26, 2020[/caption]

Hafsa Omar - Mwanza

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefanya ziara nyumba kwa nyumba katika vijiji vya Usagara na Isamilo wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Juni 26 mwaka huu, akikagua kazi ya usambazaji umeme.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isamilo, Waziri aliwaeleza kuwa lengo lake ni kufahamu idadi ya nyumba ambazo hazijaunganishiwa umeme na kujua sababu zilizofanya nyumba hizo zisiunganishwe ili kutafutia ufumbuzi suala hilo.

[caption id="attachment_53654" align="aligncenter" width="720"] Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza-kulia) akizungumza na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Isamilo, wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Restuta Wilbard, alipokwenda kukagua nyumba yake ili iunganishiwe umeme, akiwa katika ziara ya kazi, Juni 26,2020[/caption]

“Ndugu zangu wananchi, nimekuwa nikipita kwenye barabara hii mara kwa mara lakini kila nikitupa jicho mkono wa kushoto naona nyumba zenu zote hazina umeme jambo ambalo hatuwezi kulikubali,” alisema.

Akieleza zaidi, alisema kuwa mwanzoni mwa mwaka huu (2020), alitoa agizo nyumba hizo zianze kupelekewa umeme lakini mpaka sasa bado hazina umeme.

Alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwapelekea umeme wananchi hao ndani ya siku saba.

[caption id="attachment_53655" align="aligncenter" width="750"] Moja ya nyumba ambazo Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alizikagua kujua sababu za kutounganishiwa umeme hadi sasa. Waziri (hayupo pichani) alikuwa katika ziara ya kazi kijijini Usagara, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Juni 26, 2020[/caption]

Pia, aliwaagiza Maafisa Uhusiano wa shirika hilo nchini kote, kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao, kuweka umeme kwenye nyumba zao pamoja na kuwaelimisha kuhusu utaratibu wanaopaswa kufuata wakihitaji kuunganishiwa nishati hiyo.

Vilevile, aliwataka wananchi wa vijiji hivyo, kuanza mara moja kutafuta wataalamu wa kutandaza mfumo wa nyaya za umeme kwenye nyumba zao ili wapelekewe umeme kwa haraka.

Aidha, aliwataka wakandarasi wa umeme nchini kufanya kazi kwa weledi na kuonya kuwa kwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo, watasimamishwa kazi mara moja na kupewa kazi hiyo wakandarasi wenye uwezo.

“Katika Mkoa huu wa Mwanza, tumemfuta kazi mkandarasi aliyekuwepo na tumemweka mkandarasi mwingine. Tumempa hadi mwisho wa mwezi huu, awe amemaliza kazi,” alieleza Waziri.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Isamilo, Restuta Wilbard alikiri kufurahishwa na kitendo hicho cha Waziri kukagua nyumba zao na kueleza kuwa imewapa hamasa kwenda kulipia huduma ya umeme na kwamba wako tayari kupokea huduma hiyo ambayo alisema itabadilisha maisha yao kwani itawawezesha kujiajiri.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi