Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Jenista Aipongeza TCC kwa Kutekeleza Sheria za Kazi
Jul 19, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45500" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, (katikati) akiimba wimbo wa wafanyakazi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Sigara Tanzania(TCC), kutoka kulia ni Mwenyekiti TUICO-TCC, Masoud Nzowah, Katibu Mkuu, TUICO, Boniface Mkakatisi, na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu, TCC, Allan Jackson na Mkurugenzi Uzalishaji, TCC, Sam Mandera, wakati wa Hafla ya kusaini mkataba wa Hali bora mahala pa kazi kati ya TUICO na TCC iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Waziri Jenista Aipongeza TCC kwa Kutekeleza Sheria za Kazi.

Na: Paschal Dotto-MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama  ameipongeza Kampuni ya Sigara Tanzania TCC, kwa kutekeleza Sheria ya kazi baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya hali bora kazini ili kuimarisha na kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Kampuni ya sigara TCC na Chama cha Wafanyakazi Viwandani,Biashara na Taasisi za Kifedha (TUICO), Waziri Jenista alieleza kufurahishwa kwake na kampuni ya TCC kwani imezingatia na kutekeleza sheria Namba .6 ya mwaka 2004 ya  Ajira na Mahusiano kazini  na kanuni zake za mwaka 2007.

[caption id="attachment_45501" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu, TCC, Allan Jackson nakala ya mkataba wa hali bora mahala pa kazi(TCC) uliosainiwa leo Jijini Dar Salaam, Kati ya TUICO na TCC.[/caption] [caption id="attachment_45502" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimkabidhi, Katibu MKuu, TUICO, Boniface Mkakatisi, nakala ya mkataba wa hali bora mahala pa kazi(TCC), uliosainiwa leo Jijini Dar es Salaam kati ya TUICO na TCC.[/caption]

“ Sheria namba 6. ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake zimeweka muongozo wa utaratibu na njia za kufuatwa pamoja na masuala muhimu ya kuzingatia katika kufanya majadiliano mahala pa kazi, ili kudumisha uhusiano na hii ilifanyika kwa TCC na ni jambo jema sana tunawapongeza kutekeleza Sheria”, Alisema Waziri Jenista.

Waziri Jenista alisema kuwa katika kutekeleza matakwa ya Shirika la Kazi Duniani, ILO, Serikali iliweka kifungu hiki kwenye sheria zake ili kuwezesha kuwepo kwa usawa kati ya mwajiri na mfanyakazi,  kwa hiyo TCC na TUICO  wamefanya kazi nzuri itakayowezesha motisha na ari kubwa kwa wafanyakazi.

Aidha Waziri Mhagama alisema kuwa utaratibu wa kuwepo na mikataba ya mahusiano mahala pa kazi umeanza mara moja baada ya uboreshwaji wa Sheria za kazi na ajira na, TCC haikuwa nyuma mara baada ya sheria hiyo kuanza kwani mpaka sasa mkataba wa hali bora mahala pa kazi unatekelezwa na unategemea kuisha mwaka 2020 na kuruhusu makataba mpya uliosainiwa leo kuingia kazini.

Waziri Jenista  aliipongeza  timu iliyofanya majadiliano na kuwezesha kuwepo kwa mkataba uliosaniwa leo, kwani unakidhi Sheria ya Wafanyakazi na maslahi yao mahala pa kazi hususani kwa wakinamama wenye watoto.

[caption id="attachment_45503" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu TCC, Allan Jackson (kushoto) na Katibu Mkuu, TUICO, Boniface Mkakatisi(kulia), wakionyesha nakala ya Mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi(TCC), kwa wafanayakazi wa Kampuni ya Sigara Tanzania, mara baada ya kusaini mkataba huo leo Jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama.[/caption] [caption id="attachment_45504" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa TCC na TUICO mara baada ya kusaini Mkataba wa hali bora mahala pa kazi leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_45505" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Sigara ya Tanzania, TCC.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)[/caption] “ Mkataba huu wa sasa umelenga zaidi katika kutoa maslahi ya wafanyakazi wote wa TCC, hongereni sana timu iliyoongoza majadiliano na kufikia muafaka, nimefahamishwa kuwa wakina mama wanaonyonyesha wataruhusiwa kwenda Nyumbani na kupewa posho ya Shilingi 5,000 kila siku ili wawahi kunyonyesha watoto wao katika kipindi chote cha kuhudumia watoto wao kama Sheria ya Kazi na ajira inavyoeleza hongereni sana”, Alisema Waziri Jenista.

Alisema kuwa katika utekelezaji wa Sheria hiyo, TCC wameenda mbali zaidi kwa kuwajali wakina mama wenye watoto njiti, ambao  watapewa ruhusa ya kulea watoto wao huku likizo ya uzazi ikihesabiwa kuanzia pale ambapo  mtoto angezaliwa.

Alisema kuwa wakina baba mkataba huo umejikita zaidi kuwapa fursa ya likizo ya siku 10 baada ya wake zao kujifungua, lakini pia makataba huo umegusa moja kwa moja wafanyakazi wa TCC kulipiwa ada za watoto wao kiasi cha shilingo 9,000,000 kwa mwaka na aliwataka wafanyakazi watumie hela hiyo kusomesha watoto wao na sio kwa matumizi mengine.

Waziri Mhagama alitoa rai kwa waajiri wengine kuiga mfano wa TCC wa kuwajali na kuwathamini wafanyakazi mahala pao pa kazi ili kuongeza ari ya kufanya kazi na kuimarisha uzalisha wa bidhaa utaowezesha nchi kupata mapato.

Aidha Waziri huyo wa Kazi alisema kuwa TCC ni moja ya kampuni ambayo inatekeleza kwa vitendo Sera ya Awamu ya Tano ya kuijenga Tanzania ya Viwanda kwani mkataba huo utaongeza nguvu ya kujituma kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, TUICO, Boniface Mkakatisi alisema kuwa kampuni ya Sigara Tanzania inamahusiano mazuri na wafanyakazi wake ndiyo maana wameweza kufikia makubaliano hayo ambayo yana tija kwa pande zote mbili.

“Hapa ni mahali ambapo Ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi ni mkubwa sana na ndiyo maana mimi ni fundi wa kuongoza migomo lakini hapa nimeshindwa kwa sababu wanashirikiana hawafarakani, pia wanafanyakazi kwa bidii kubwa hivyo migomo haiwezekani na kwa mkataba huu ndiyo basi kabisaa”, Alisema Katibu Mkuu. Huyo wa TUICO.

Naye Mkurugunzi Mkuu, TCC, Alllan Jackson, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa Ushirikiano wakati akiwa hapa nchini na amempongeza Rais  Magufuli kwa hatua  anazochukua katika kuijenga Tanzania ya Viwanda.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi