[caption id="" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha redio Jamii cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) chenya masafa ya 92.1 leo Jijini Arusha.[/caption]
Na Lorietha Laurence-WHUSM, ARUSHA
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua kituo cha Redio Jamii cha TBC chenye masafa ya 92. 1 ambacho kimegharimu jumla ya milioni 627 leo Jijini Arusha.
Wakati wa uzinduzi huo Mhe. Dkt. Mwakyembe amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa kituo hicho cha redio ni kuhabarisha umma wa Arusha na mikoa ya jirani fursa mbalimbali zinazopatikana katika Jiji hilo ukizingatia chanzo kikuu cha mapato yake yanatokana na Utalii wa ndani.
“Ni matarajio yangu redio hii itakuwa mstari wa mbele katika kutangaza na kueleza fursa mbalimbali zinazopatikana katika Jiji la Arusha pamoja na kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi” amesema Mhe.Dkt. Mwakyembe
[caption id="" align="aligncenter" width="800"]Aidha ameeleza kuwa TBC kama Shirika la Umma halina budi kuhakikisha inatoa matangazo ya uhakika na ukweli kwa kuifikia jamii kubwa zaidi hususani zile za vijijini ambako vyombo vingine vya habari havijaweza kuwafikia.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqqaro ameushukuru uongozi wa TBC na Serikali kwa ujumla kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa kituo cha redio jamii kwa ukanda wa kaskazini.
“Redio hii ya Jamii ni muhimu sana kwa watu wa Ukanda wa Kaskazini ukizingatia asilimia 80 ya mapato yake yanatokana na sekta ya utalii hivyo itatupa fursa ya kujitangaza zaidi” alisema Bw. Daqqaro.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya TBC na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ameeleza kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linahitaji uwekezaji mkubwa ili kufika maeneo mengi zaidi nchini.
Vilevile Mkurugenzi Mkuu Shirika La Utangazaji La Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa Redio jamii iliyofunguliwa rasmi leo Jijini Arusha ni mkakati wa Serikali kuwafikia wananchi wengi mahali popote walipo.