Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Bashungwa Atoa Wito kwa Wadau wa Michezo Kuhamasisha Chanjo ya UVIKO 19
Sep 03, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Na, Projestus Binamungu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa vilabu vyote 16 vya mchezo wa soka nchini kuhamasisha wachezaji wake, viongozi na mashabiki kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 ili kulinda afya zao na kulinda afya za watanzania wengine.

Waziri Bashungwa ametoa rai hiyo jana Septemba 1, Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mchezo wa kirafiki kati ya viongozi wa dini (Kamati ya Amani) na wachambuzi wa habari za michezo, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamanzi jijini Dar es Salaam.

 “Mimi kama Waziri mwenye dhamana kwenye sekta hizi nitaendelea kushirikiana na wadau wote katika kutoa elimu na hamasa kwa watanzania wenzetu kuhusu umuhimu wa kupata chanzo dhidi ya Uviko 19”. Amesisitiza Mhe. Bashungwa

Amewashukuru viongozi wa dini na wachambuzi wa michezo kwa kuandaa na kushiriki katika mchezo huo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya Uviko 19.

Katika mchezo huo timu zote zimetoka suluhu kwa kufungana magoli tatu kwa tatu huku kila upande ukimpongeza mpinzani wake kwa umahiri.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi