Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watumishi Wetu Tunaendelea Kuwafundisha - Dkt. Ibenzi
Aug 09, 2023
Watumishi Wetu Tunaendelea Kuwafundisha - Dkt. Ibenzi
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Hospitali hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Agosti 9, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
Na Ahmed Sagaff - MAELEZO

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi amesema watumishi wa hospitali hiyo wanaendelea kupata mafunzo sehemu mbalimbali ikiwemo nje ya nchi.

Akizungumza leo katika Ukumbi wa Idara ya Huduma za Habari jijini Dodoma, Dkt. Ebenzi amesema mafunzo yanawasaidia kujua teknolojia mpya ili kuendeleza juhudi za kuboresha huduma hospitalini hapo.

"Mkiona hospitalini pamejaa wanafunzi msishangae, tuna wanafunzi wanaokuja kwa mafunzo, wale ni madaktari wenzetu, wale ni wauguzi wenzetu, tunawafunza kutibu kwa vitendo, hatuwaruhusu kutibu wakiwa peke yao," ameeleza Dkt. Ibenzi.

Aidha, Daktari huyo amearifu kwamba hospitali yao inaendelea kutatua changamoto mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.

"Tunataka wateja wetu wapate huduma bila changamoto yoyote, dawa zote tunazo hospitali, hutokea bahati mbaya dawa hamna labda inapatikana Kenya, huwa tunawapa wagonjwa siku mbili waje wachukue," amesema Dkt. Ibenzi.

Kuhusu changamoto ya msongamano wa wagonjwa kwenye wodi ya watoto ambapo watoto hulazwa wawiliwawili katika kila kitanda, Dkt. Ibenzi ameeleza kwamba tatizo hilo litakwisha ndani ya wiki mbili zijazo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi