Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watumishi NAOT Waaswa Kuzingatia Maadili
May 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_43033" align="aligncenter" width="900"] Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akisisitiza umuhimu wa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao , ameyasema hayo wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Wameaswa Kuziungatia Maadili wakati wote Wanapotekeleza majukumu yao ili kuendana na dhamira ya Serikali kufikia maendeleo endelevu na uchumi wa kati.

Akizungumza wakati akizindua Baraza jipya la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael amesema watumishi wote wa Ofisi hiyo wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia sharia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuleta tija katika majukumu wanayotekeleza.

[caption id="attachment_43034" align="aligncenter" width="900"] Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisisitiza umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi wakati wa hafla ya kufungua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43035" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Mwenwejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akikata utepe kuzindua mkataba wa huduma kwa wateja wakati wa hafla ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption]

“ Sitarajii Wakaguzi wetu Wakawa miongoni mwa watumishi watakaokumbwa na kashfa za namna yoyote hivyo niwaase kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu,kudai na kupokea rushwa” Alisisitiza Dkt. Michael

Akifafanua amesema kuwa hatma ya makosa hayo ni kupoteza ajira na kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakama ili sharia iweze kuchukua mkondo wake hali inayoweza kupelekea mhusika kufungwa jela.

Aidha, aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kutumia fursa za Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali kujiletea maendeleo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ardhi.

[caption id="attachment_43038" align="aligncenter" width="900"] Naibu mkaguzi wa NAOT ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Bi Wendy Masoy akitoa neno la shukrani baada hafla ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43039" align="aligncenter" width="715"] Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Mwenwejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akisisitiza jambo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad leo Jijini Dodoma baada ya kuzindua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo.

[/caption] [caption id="attachment_43040" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa baraza hilo leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43036" align="aligncenter" width="900"] Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akiteta jambo na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Mwenwejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michaelwakati wa hafla ya kufungua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43037" align="aligncenter" width="900"] Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) mara baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali Prof. Mussa Assad amesema kuwa Ofisi hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa weledi ili kutimiza lengo la kuanzishwa kwake ikiwemo kuhakikisha kuwa ripoti ya ukaguzi inatolewa kama inavyotakiwa kila ifikapo mwezi machi.

Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo wameendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii nyakati zote hali inayoonesha jinsi wanavyojitoa katika kuhakikisha kuwa kazi za ofisi hiyo zinafanyika kama inavyotakiwa.

Baraza la wafanyakazi wa NAOT linafanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili likiwa na dhamira ya kuwaleta pamoja wajumbe kutoka katika Idara, Vitengo, Kada, baadhi ya Taasisi na vyama vya wafanyakazi likiwa ni Baraza la mwaka 2018/2019.

(Picha zote na Frank Mvungi)

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi