Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watoto 28 Wafanyiwa Upasuaji wa Moyo wa Kufungua Kifua
Oct 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_17207" align="aligncenter" width="750"] Afisa Muuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus na Arianna Minghetti wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimnywesha maziwa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo bila ya kufungua kifua (Catheterization) katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.[/caption] [caption id="attachment_17208" align="aligncenter" width="750"] Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua na kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.[/caption] [caption id="attachment_17209" align="aligncenter" width="750"] Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Mending Kids la nchini marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) na kuzibua mishipa ya Moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.[/caption] [caption id="attachment_17212" align="aligncenter" width="750"] Maafisa Uuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwezao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakijadiliana kuhusu maendeleo ya wagonjwa waliolazwa katika chumba hicho baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri. (Picha na JKCI)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi