Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Watakiwa Kuepuka Kitambi na Uzito Uliokithiri.
May 19, 2017

[caption id="attachment_1295" align="aligncenter" width="1000"] Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Mashombo Mkamba akielezea jambo kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige[/caption] Na: Nuru Juma-MAELEZO. Daktari Mshauri kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) Dkt. Ali Mzige amewataka watanzania kuepuka uzito mkubwa na kitambi ili kufanya miili yao kukaa mbali na magonjwa yanayosababishwa na vitu hivyo. Dkt. Mzige amezungumza hayo leo katika ukumbi wa maelezo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari. Aliongeza kuwa watu wengi wanachukulia kawaida na wengine wanapenda kuwa na kitambi na uzito mkubwa lakini ni vitu vyenye madhara makubwa na husababisha magonjwa ambayo ni magumu kutibika. “Unene uliokithiri huleta shida kwenye moyo, shinikizo kubwa la damu,kisukari, saratani za aina mbalimbali, kushindwa kupumua vizuri na magonjwa mengine mengi hivyo watu wanatakiwa kuepuka ili kujinusuru na magonjwa hayo,” alisema Dr Mzige.   [caption id="attachment_1297" align="aligncenter" width="750"] Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA).[/caption] [caption id="attachment_1300" align="aligncenter" width="1000"] Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige akionyesha Jarida linaloandaliwa na Shirika la Afya Duniani wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Mashombo Mkamba.
Picha na: Frank Shija[/caption] Aliongeza kuwa tafiti zinaonyesha asilimia kubwa wanawake  wanavitambi na uzito uliokithiri kuliko wanaume hali inayotokana na wanawake wengi kupendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi. Aidha aliwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kula vyakula vya asili,kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara ili kujua mapema kama ana tatizo lolote la kiafya na kujiepusha na maradhi yanayoweza kuepukika. Aliongeza kuwa uzito wa mtu unatakiwa kulingana na umri na urefu kwani mtoto wa mika 5 anapaswa kuwa na kilo 18, kijana mwenye miaka 14 mvulana kilo 48 na msichana kilo 49 huku mtu mzima mwanaume mwenye urefu wa futi 5 na inchi 8 anapaswa kuwa na kilo 68. Tiba nzuri na iliyosahihi ya kuepuka maradhi mengi ni kutokaa masaa 4 bila kufanya kazi,kuzuia kitambi kisijitokeze kwa kula kiasi cha chakula kinacholingana na mahitaji yako, kupunguza ulaji wa sukari na mafuta na kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.

Mipangilio
Marekebisho ya Lugha
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi