Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Waaswa Kutunza Misitu
Aug 17, 2023
Watanzania Waaswa Kutunza Misitu
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji na mafanikio ya wakala hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23 na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Na Na Mwandishi wetu

Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo ametoa wito kwa jamii kutunza na kuhifadhi rasilimali za misitu kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vya baadae.

Prof. Silayo ametoa wito huo Agosti 16, 2023 jijini Dodoma wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji na mafanikio ya wakala hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23 na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2023/24.

“Niombe jamii iwe nasi katika safari hii ya uhifadhi wa rasilimali za misitu kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vya baadae, tujiepushe kuchoma moto misitu, uvunaji haramu na twende na kauli mbiu ya Achia Shoka Kamata Mzinga,” amebainisha Prof Santos.

Aidha amesema, Sekta ya Misitu na Nyuki nchini ni muhimu kutokana na mchango wake mkubwa katika ukuaji wa sekta nyingine za uzalishaji kama vile utalii, maji, kilimo, mifugo na nishati pamoja na sekta ya viwanda, hivyo kutokana na umuhimu huo, uhifadhi wa rasilimali za misitu ni jukumu la msingi na linapaswa kupata mchango kutoka kwa wadau wote.

TFS imekuwa ikisimamia rasilimali mbalimbali nchini ikiwemo rasilimali za misitu na nyuki, vituo vya ukusanyaji wa mbegu za miti na rasilimali za malikale na pia kuhakikisha uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki na upatikanaji wa bidhaa za mazao ya misitu na nyuki nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi