[caption id="attachment_23013" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa benki hiyo Bw. Johnson Nyera akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu barani Afrika iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei Bibi. Ruth Minja na Mwakilishi wa Asasi za Kiraia Bw. Stephen Chacha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".(Picha na: Frank Shija)[/caption]
Na: Eliphace Marwa
WATAKWIMU nchini watakiwa kuimarisha mbinu za uzalishaji wa takwimu kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kusaidia katika ukusanyaji na upatikanaji wa takwimu bora zitakazosaidia kupanga mipango ya maendeleo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika na kuwataka wadau waliopo kwenye mfumo wa utoaji na utumiaji wa takwimu kushirikiana ili kupunguza kukosekana kwa ulinganifu wa takwimu.
[caption id="attachment_23014" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa akisisitiza jambo wakati wa hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya, Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa benki hiyo Bw. Johnson Nyera, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".[/caption] [caption id="attachment_23015" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid akitoa neno la shukrani katika hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki hiyo Bw. Johnson Nyera, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".[/caption] [caption id="attachment_23016" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bibi. Elizabeth Talbert akizungumza katika hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".[/caption]“Matumizi ya teknolojia yataipunguzia Serikali gharama za uzalishaji wa takwimu na kuongeza ubora kutokana na mahitaji makubwa ya takwimu kwa matumizi mbalimbali,” alisema Bw. Nyala.
Nyila aliongeza kuwa takwimu bora za uchumi ni muhimu katika kupanga mipango ya maendeleo na utungaji wa sera kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi.
“Wakati nchi mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania zimeanza kutekeleza agenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, mahitaji ya takwimu bora za uchumi yanahitajika sana,” alisema Bw. Nyila.
[caption id="attachment_23017" align="aligncenter" width="750"] Afisa Habari Mwandamizi Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Said Ameir ambaye alikuwa mshereheshaji katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika akifafanua baadhi ya mada zilizowasilishwa katika hmaadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".[/caption] [caption id="attachment_23018" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa akifafanua jambo wakati wa hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".[/caption] [caption id="attachment_23019" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia majadiliano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwl. Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.[/caption]Kwa upande wake Mkurugezni Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alisema kuwa madhumuni makubwa ya kuadhimisha siku hii ni kuongeza uelewa wa umma juu ya umuhimu wa takwimu katika nyanja zote za kimaisha ya kijamii na kiuchumi.
Aliongeza kuwa nchi mbalimbali za Afrika zilikubaliana kuadhimisha maadhimisho hayo kutokana na uhitaji mkubwa wa ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa takwimu za uchumi katika kuelekea utekelezaji wa Agenda ya Afrika ya mwaka 2063 na malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.
[caption id="attachment_23020" align="aligncenter" width="750"] Mwanafuzni wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu Bi. Felister Mande akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa baada ya kuwa mshindi wa pili katika shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa hiyo Bw. Johnson Nyera, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid na Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya.[/caption] [caption id="attachment_23022" align="aligncenter" width="683"] Mwanafuzni wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu Bi. Edda Magesa akipokea zawadi ya shilingi laki tatu kutoka kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Uchumi wa BoT Bw. Johnson Nyera baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".Kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid na Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya.[/caption] [caption id="attachment_23023" align="aligncenter" width="750"] Mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Johnson Nyera akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi washindi wa shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" wakati wa maadhimisho hayo leo Jijini Dar es Salaam. Wanafunzi kutoka kushoto ni Edda Magesa (mshindi wa kwanza), Fred Komba (mshindi wa tatu) na Felister Mande (mshindi wa pili).[/caption] [caption id="attachment_23024" align="aligncenter" width="750"] Mgeni rasmi wa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Johnson Nyera akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Shule za Sekondari Kisutu Wasichana na Azania walioshiriki shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" wakati wa maadhimisho hayo leo Jijini Dar es Salaam. Wanafunzi kutoka kushoto ni Edda Magesa (mshindi wa kwanza), Fred Komba (mshindi wa tatu) na Felister Mande (mshindi wa nne).(Picha na: Frank Shija)[/caption]Dkt. Chuwa aliongeza kuwa Takwimu za kiuchumi pia ni muhimu kwa Tanzania katika kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kufikia nchi ya kipao cha kati kupitia ujenzi wa viwanda, ambayo huchangia wastani wa asilimia 6.5 katika pato la taifa.
Siku ya Takwimu Duniani huadhimishwa tarehe 20 Oktoba katika kipindi cha kila miaka mitano ambapo kwa mwaka huu maadhimisho haya yameongozwa na Kauli mbiu isemayo “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora”.