Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wataalam wa Utawala Bora AU Wapongeza Utendaji wa JPM
Jul 18, 2017
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tawi la Tanzania, Rehema Twalib (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo hii jijini Dar es salaamjuu ya uzinduzi wa ripoti ya APRM kuhusu utawala bora nchini. Kulia ni Mratibu wa APRM kutoka Makao Makuu Dr. Rachel Mukamunana. (Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO)

Na. Bushiri Matenda na Immaculate Makilika- MAELEZO

Wataalam wa Mpango wa Kijitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM) wameelezea kuridhishwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli Katika kusimamia misingi ya Demokrasia na Utawala Bora nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Tathmini za Utawala Bora kwa Nchi za Afrika katika Sekretarieti ya APRM iliyoko Nidrand Afrika Kusini na Mratibu wa Mchakato wa Tanzania, Dkt. Rachel Mukamunana alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa ripoti ya APRM utakaofanywa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan siku ya Jumatano.

Dkt. Rachel alisema kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa masuala yanayohusu utawala bora ikiwemo kutatua kero mbalimbali zikiwemo zile za masuala ya muungano.

“Serikali ya Rais Magufuli imeonesha kujitoa kwa dhati katika kusimamia masuala ya utawala bora ikiwemo uwajibikaji na uzinduzi wa ripoti hii ni kiashirio tosha cha dhamira ya Serikali katika kusimamia misingi ya utawala bora,” alieleza.

Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tawi la Tanzania, Rehema Twalib (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo hii jijini Dar es salaamjuu ya uzinduzi wa ripoti ya APRM kuhusu utawala bora nchini. Kulia ni Mratibu wa APRM kutoka Makao Makuu Dr. Rachel Mukamunana. (Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO)

Kutokana na kujitoa huko, Dkt. Rachel alisema anatarajia kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizoainishwa katika ripoti hiyo ya mwaka 2012 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa kesho (leo).

Nae Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Rehema Twalib alieleza kuwa ripoti hiyo imeanisha sifa ambazo Tanzania imekuwa ikisifiwa nazo kuwa ni pamoja na kudumisha amani na umoja, kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50 sasa, pamoja na uboreshwaji wa utoaji huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, usawa wa kijinsia na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Alibainisha sifa zingine zilizotajwa kwa mujibu wa Mpango huo wa AU kuwa ni kulinda haki za binadamu, matumizi ya lugha, moja ya Kiswahili na hatua za maendeleo ya kiuchumi nchini.

Katibu huyo alisema uzinduzi wa ripoti ni utekelezaji wa mojawapo ya matakwa ya kiutaratibu katika mchakato wa APRM, ikiwa ni kiashiria kimoja wapo cha utekelezaji rasmi wa yale yaliyoandikwa kwenye ripoti pia kielelezo cha utayari wa Serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tawi la Tanzania, Rehema Twalib (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo hii jijini Dar es salaamjuu ya uzinduzi wa ripoti ya APRM kuhusu utawala bora nchini. Kulia ni Mratibu wa APRM kutoka Makao Makuu Dr. Rachel Mukamunana. (Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO)

Rehema alieleza kuwa lengo la APRM ni kuzisaidia nchi za Kiafrika, Tanzania ikiwa mwanachama mmoja wapo, kuhakikisha kuwa zinaimarisha utawala bora kwa kuwashirikisha wananchi wao kubainisha changamoto zao ili kuzigeuza kuwa fursa za maendeleo na mambo mazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchi yenyewe na hata kwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

APRM Tanzania ilipewa dhamana na Serikali ya Jamhuru ya Muungano nwa Tanzania kusimamia majukumu ya nchi katika kuratibu tathmininya utawala bora kwa mujibu wa muongozo wa Wakuu wa Nchi za Kiafrika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi