Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Uyui Waipongeza Serikali ya Awamu ya Tano
May 18, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_43154" align="aligncenter" width="750"] Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka MKURABITA Bw. Antony Temu akisisitiza kuhusu umuhimu wa mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima waliorasimisha mashamba yao Wilayani Uyui na kupatiwa hati za haki milki za kimila za kumilki ardhi.[/caption]

Na Frank  Mvungi

Wananchi Wilayani Uyui mkoani Tabora Wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwawezesha kurasimisha mashamba yao na kupatiwa hati za haki milki za kumiliki ardhi hali inayowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza wakati wa mahojiano maalum Wilayani humo akiwemo mkazi wa  Miyenze Bw. Julius Magoi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha dhamira ya dhati kuwawezesha wananchi Vijijini kupitia Mpango wa Kurasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

“ Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuwezesha MKURABITA kuturasimishia mashamba yetu, kuyapima na kupatiwa hati za haki milki za kimila hali inayotuwezesha kuongeza tija katika uzalishaji mashambani hasa katika mazao ya biashara” Alisisitiza Bw. Magoi

Akifafanua amesema kuwa MKURABITA imeendesha mafunzo  yanawawezesha wakulima kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwakwamua wananchi wanyonge hasa wanaoishi vijijini katika Wilaya hiyo kwa kuwajengea stadi za kilimo bora, ufugaji wa kuku kibiashara, kilimo cha pamba, alizeti na mazao mengine .

[caption id="attachment_43153" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora mhe. Gift Msuya akifungua mafunzo kwa wakulima wa Kata ya Miyenze Wilayani humo hivi karibuni, mafunzo hayo yakuwajengea uwezo wakulima waliorasimisha mashamba yao Wilayani humo na kupatiwa hati za haki milki za kimila za kumilki ardhi yamefanyika katika Kata za Miyenze na Lutende.[/caption]

Kwa upande wake mkazi mwingine wa Kata hiyo  Bi Nyamizi Shija amesema kuwa anamuomba Rais Magufuli aendelee na jitihada zake za kuwawezesha wananchi kama ambavyo anafanya sasa kwa kuwa wanaendelea kumuunga mkono katika kila jambo analofanya ili kuwaletea maendeleo.

Aliongeza kuwa utendaji mzuri wa Serikali ya Awamu ya Tano umewawezesha wananchi kunufaika na rasilimali za nchi yao ikiwemo kutolewa kwa fedha zinzoelekezwa Vijijini kuwajengea uwezo akitolea mfano urasimishaji wa ardhi ambayo ni nyenzo kuu ya kuwawezesha wananchi.

Naye mkazi wa Kata ya Lutende Bw. Omari Mohamed amesema kuwa Serikali imeonesha kuwajali, kuwatambua, kuwathamini na kuwawezesha wananchi vijijini kwa kuwa inachukua hatua kuimarisha sekta zenye kuwainua wananchi ikiwemo kilimo na mifugo hali itakayowezesha kufikiwa kwa malengo yakutukwamua kiuchumi kama wakulima.

“Rais Magufuli yuko makini, anatetea wanyonge na anaelewa mahitaji ya wananchi tunaoishi vijijini ndio maana tumepata fursa ya kujengewa uwezo kupitia MKURABITA na kurasimishiwa mashamba yetu hali iliyotuwezesha kupata hati za haki milki za kimila za kumiliki ardhi ambazo tutazitumia kujikwamua kiuchumi” Alisisitiza Mohamed

Akifafanua Mohamed amesema kuwa wananchi wanaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea maendeleo.

[caption id="attachment_43155" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora mhe. Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi waliopatiwa hati za haki milki za kimila za kumiki ardhi Wilayani humo hivi karibuni wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo yaliyowanufaisha wakulima zaidi ya 200 katika Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuwakwamua kiuchumi wakulima hapa nchini.[/caption]

Kwa upande wake Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka MKURABITA Bw. Antony Temu amebainisha kuwa wananchi wa Kata za Miyenze na Lutende wamejengewa uwezo wa kutekeleza kilimo chenye tija cha mazao ya biashara kama alizeti, pamba na mengine ili waweze kuzalisha kwa tija.

Aliongeza kuwa mada nyingine walizofundishwa wakulima hao ni pamoja na utunzaji wa mazingira, utunzaji wa kumbukumbu, fursa zilizopo katika taasisi za fedha, uandaaji wa mpango wa biashara na uanzishaji wa vyama vya ushirika.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi waliorasimisha mashamba yao na kupatiwa hati za hakimilki za kimila yamefanyika katika Kata ya Miyenze na Lutende Wilayani Uyui mkoani Tabora na kushirikisha wakulima zaidi ya 200.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi