Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wanachi Waaswa Kutunza Mazingira
Mar 23, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na  Mwandishi Wetu

Mradi  wa kuchakata majitaka kiasi cha lita elfu 10,000 kwa siku kuwanufaisha  wakazi wa mburahati na maeneo ya jirani  ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kutunza mazingira na kuimarisha huduma kwa wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati  wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji kwa niaba ya Mkuu wa  Mkoa wa Dar es salaam mkuu wa Wilaya ya Ubungo mhe.  Kisare Makori amesema amefurahishwa kusikia kuwa katika wiki ya maji mkoa umeshiriki katika shughuli za upandaji miti katika chanzo cha maji Ruvu.

"Kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosisitiza kuhusu kuhifadhi vyanzo vya maji na mifumo ya ikolojia kwa maendeleo ya Jamii hivyo tunao wajibu wakusimamia suala hili" alisisitiza Kisare

Akifafanua zaidi Kisare amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wakazi wa Dar es Salaam wanapata huduma bora ambapo maji yatakayochakatwa yatasaidia kuondoa tatizo la magonjwa ya milipuko kama kipindupindu .

Aidha, maji yatakayochakatwa yanaweza kutumika katika kilimo cha mbogamboga za uzalishaji wa gesi kwa matumizi ya majumbani.

Mradi huo wa kuchakata majitaka unajengwa na Asasi ya Kijerumani ya BORDA kwa ushirikiano na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, DAWASA na Mkoa wa Dar es salaam.

Awali akitoa maelezo kuhusu mradi huo mwakilishi kutoka shirika la BORDA alisema hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu shilingi milioni 95 na kuwa gharama za kujenga uwezo, uhamasihsaji wa jamii kuweka mfumo bora wa usimamizi unatarajiwa kufikia shlingi milioni 90.

Alitaja faida za mradi kuwa ni pamoja na kuweza kuondoa matatizo yatokanayo na uchafuzi wa Mazingira, kurahisisha upatikanaji wa huduma ya uondoshwaji wa majitaka kwa gharama nafuu, upatikanaji wa gesi kiasi cha lita  7000 kwa siku , kupatikana kwa maji na mbolea kwa ajili ya bustani kuzunguka eneo la mradi.

Sherehe za kilele cha wiki ya maji zimehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Theresia Mmbando,  Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika viwanja vya Mburahati Barafu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo aliweka jiwe la msingi la mradi huo na kuhudhuriwa na viongozi wa Halmashuri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni, na Ubungo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi