[caption id="attachment_49517" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.[/caption]
Na Judith Mhina
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrisom Mwakyembe amezindua kitabu cha Gender and Media Handbook in Tanzania wakati wa maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano.
Akizindua kitabu hicho katika ukumbi wa Kibo ndani ya hoteli i ya Kimataifa ya Hyatt Regence - The Kilimanjaro leo Jijini Dar-es-salaam Waziri Dkt Mwakyembe amesema “Wana habari mtakuwa vibarua mpaka lini”.
Hebu tujaribu kutekeleza sheria mbili ya Habari na ile ya haki ya kupata taarifa, ambapo Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo zimeiga kiila kitu kilichoandikwa kwenye sheria husika ya kimataifa, badala yake wanaleta mada yao pendwa ya jinsia moja, hatuwezi kukubali. Amesema Waziri Mwakyembe.
Akijibu risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano- Tanzania Women Media and Public Relation Networ,. Bevin Bhoke Chacha Mwita ambaye amesema kuwa waandishi wa habari wanawalke wananyanyaswa kijinsia katika vyumba vya habari . Hii ikiwa ni pamoja na kutolipwa mshahara stahiki kulingana na sifa walizonazo, kutopandishwa madaraja, lugha chafu na kubaguliwa katika majukumu ya kazi kama waandishi wa kiume na kujikuta wengi wao wakiwa waadhirika wa kunyanyaswa kijinsia.
Waziri mwakyembe aliongeza kwa kusema “Tunaomba wahisani watenge nusu ya fedha wanazotoa ili kuangalia masilahi ya waandishi wa habari na kuboresha mazingira ya kazi kutokana na kuwa na vitendea kazi duni katika vyombo vyao vya Habari.
Ninashangaa waandishi wa Habari ambao wanashangilia kuwa na taaluma isiyo na mpangilio, sheria wala kanuni, katika kuimarisha taaluma yao na ndio maana leo hii mnalalamika masilahi madogo yasiyolingana na kazi mnayofanya au hatopata mishahara kabisa .
[caption id="attachment_49518" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa UN Women Nchini, Bi. Hodan Addou akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.[/caption]Akisisitiza jambo hilo Waziri amesema “Ni agfadhali kuwa na vyombo vya Habari vichache vinavyojali na lulinda masilahi ya Waandishi wa Habari kuliko kuwa na vyombo vingi ambavyo , haviangalii masilahi ya waandishi wa Habari, kuwalipa mishahara stahiki kwa wakati .
Akitoa agizo kwa kukabiliana na suala la kupiga vita unyanyasaji kijinsia Waziri Mwakyembe amesema kuwa nimefurahi kwa kuwa mmeonyesha namba mbili maalum za simu ambazo yeyote atakayenyanyaswa kijinsia azipige ili kupata msaada. Aidha, Wizara yangu naiagiza kuwa na namba maalum ya simu ambayo mtanipigia mimi moja kwa moja na kuwatangaza wale wote wanaomnyanyasa wanahabari wanawake ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwenye vyumba vya habari.
Akisisitiza agizo hilo amesema dirisha la Waziri lipo wazi kwa kila mtu bila mashariti yeyote na naomba wanahabari walitumie kweli kweli, mimi nikiwa kama mzazi na kiongozi ni lazima kuhakikisha suala hili linakuwa historia.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa wanahabari wanawake na maafisa uhusiano Bi Chacha ameongeza kwa kusema kuwa wanawake wana
Katika hizi siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika vyumba vya Habari Mshauri wa masuala ya wanawake wanahabari Bi Pili Mtambalike amesema “Wanahabari wanawake wananyanyaswa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa kupewa kazi nyepesi ikilinganiswha na waandishi wa kiume katika vyombo vya habari kutokana na kutokujiamini
[caption id="attachment_49519" align="aligncenter" width="750"] Mwandishi wa Habari Mkongwe, Pili Mtambalike akichangia mada katika Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.[/caption]Aidha , katika vyombo vingi vya Habari utafiti unaonyesha kuwa wahariri wengi ni wa jinsia ya kiume japo wapo wanawake ambao wanastahili kuwa wahariri na wanalingana hata kwa taaluma walizonazo ila hawapewi madaraka na hata hawapandishwi madaraja kama wenzao wa jinsia ya kiume.
Vilevile waandishi wanahabari wachanga wakike wananyanyaswa kingono na waliowengi wanafanya kazi kwenye vyombo hivyo kama correspondence na kulipwa kulingana na stori ambayo haiwatoshelezi kimaisha. Pia, Lugha wanazotumia wahariri katika vyumba vya habari ni lugha chafu za kudhalilisha na vitisho.
Akiongelea upande wa pili kama ushauri kwa wanahabari wachanga wanawake amesema kuwa ipo tabia ya wanahabari hawa wa kike wachanga kujiendekeza ili wapate wepesi wa kufanya kazi bila kuwa wabunifu kujituma na kuhakikisha wanajifunza kila mara ili kukomaa kitaaluma.
Pili Bi Mtambalike amesema kuwa ipo haja ya kuwa na sera ya jinsia katika vyombo vya Habari na kuhakikisha sera hizo zinatumika . Utafiti uliofanywa katika vyombo 23 vya Habari sita tu ndio vilikuwa na sera inayoeleweka ambayo haitumiki.
Hivyo tunaomba Jukwaa la Wahariri Tanzania –TEF liangalie namna gani linaweza kuleta usawa wa kijinsia katika kuwa na idadi sawa ya wahariri kwa kuwa wanawake walio wengi wanaishia katika ngazi ya Wahariri wasaidizi . Akitoa Takwimu amesema asilimia 26 ya wanawake ndio wahariri wasaidizi waliosalia wote ni jinsia ya kiume wakiwemo wahariri wakuu wa jinsia ya kiume.
[caption id="attachment_49520" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe, akikata utepe kuzindua kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari katika jukwaa la Waandishi wa habari wanawake, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.[/caption]Pia, unyanyasaji huu wa wanawake unafanyika hata kwenye upande wa vyanzo vya Habari ambavyo kwa wanawake ni asilimia 36 ,a silimia 64 ya vyanzo vya Habari hutokana na wanaume. Hivyo tunaomba hata wanawake wanahabari walione hili na kuhakikisha wanawahoji wanawake wenzao kama chanzo cha Habari badala ya kujikita zaidi kwa wanaume. Amesema Bi Mtambalike.
Naye Mhariri Mtendaji Bakatri Machumu ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo na kuwasilisha taarifa yake kupitia video iliyorekodiwa amesema kuwa kutokana na uzoefu wangu katika tasnia ya Habari waandishi wanawake ni wabunifu na wananafasi kubwa ya kuangalia wanawake ambao wako katika jamii na kusaidiana.
Naye Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bibi Hodan Addou amesema “ Vyombo vya Habari ni kati ya vyombo vyenye nguvu kubwa hivyo vitumike katika kuhakikisha vinaondoa kabisa suala zima la unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia katika vyomvo vya Habari”.
[caption id="attachment_49521" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe na Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, wakionyesha nakala ya kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari, kilichozinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Jukwa la Waandishi wa Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.[/caption]Pia, ameongeza kwa kusema kuwa ni lazima kuhakikisha wanahabari wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanatumia taaluma yao bila vikwazo ili kuwaletea maendeleo mtu momoj ammoja na Taifa kwa ujumla.
Akiongelea kauli mbiu ya mwaka katika maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano. Unaosema “Changamkia Fursa sasa” Grabbing Opportunity now Katibu wa Kamati Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano, Bi Leah Mushi amesema nafasi za mafunzo ambazo hutolewa na wadau mbalimbali wa sekta wa Habari wakiwemo Wanawake wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Shirika la Mitandao ya Habari- Internews.
Aidha, kuna fursa nyingi za mafunzo ya Mitandao ya kijamii na pia wanatoa vitendea kazi kwa waandishi wachanga wake kwa waume ili waweze kujitegemea katika kufanya kazi zao na kujiendeleza kitaaluma.
Naye Afisa Uhusiano wa Kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bi Stela Vuzo, amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa wanahabari wachanga wanawake Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya kusimamia taaluma ya Habari na kujiendeleza, ikiwa ni pamoja na kupata kazi sehemu mbalimbali duniani na kuacha kulalamika kuhusu masilahi na mishahara midogo.
[caption id="attachment_49522" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, akiandika anayoyasikia wakati wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.[/caption]Haya tunayoyaona sasa inatokana na mfumo dume ambao tumeuishi kwa miongo kadhaa ambayo adhari zake zinajitokeza , hivyo sio kitu cha ajabu katika jamii zetu, na hayatokei kwenye tasnia ya Habari peke yake bali ni mfumo wa malezi kwenye jamii zetu ambao unatakiwa ukemewa, upigwe vita na uache kubagua mtoto wa kike na yule wa kiume. Amesema Mhariri Jesse Kwayu.
Iko haja ya Wadau wa Tasnia ya Habari kuongeza kwa pamoja na kuona umuhimu wa sheria , kanuni na taratibu tulizojiwekea ili kuifanya sekta ya Habari iwe na mfumo madhubuti unaowafaidisha wana taaluma ya Habari kwa jumla.