Wakuu wa Wilaya Watembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango Nanenane, Mbeya
Aug 06, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Bw. Onesmo Buswelu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bw. Filberto Sanga (wa pili kushoto) wakimsikiliza Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Kitengo cha Pensheni Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Haruna Sempombe, akifafanua utaratibu wa malipo ya mafao na mirathi, walipotembelea banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa Uwanja wa John Mwakangale, jijini Mbeya. Kulia ni Mhasibu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Joyce Memba.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Bw. Onesmo Buswelu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bw. Filberto Sanga (wa pili kushoto) wakijadiliana na Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa SELF, Bi. Linda Mshana kuhusu mikopo inayotolewa na Mfuko huo kwa vikundi mbalimbali vikiwemo wakulima, wajasiriamali, wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na vikundi vya wanawake, walipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa uwanja wa John Mwakangale, jijini Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Bw. Onesmo Buswelu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bw. Filberto Sanga (wa pili kushoto), wakisikiliza maelezo ya uwekezaji kwenye Hati Fungani na Hisa kutoka kwa Afisa Mipango – Mwandamizi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), Bw. Godfrey Laurent Makoi, walipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa Uwanja wa John Mwakangale, jijini Mbeya. Kulia na Bw. Christopher Ngonyani.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Bw. Onesmo Buswelu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bw. Filberto Sanga (wa pili kushoto), wakimsikiliza Meneja Masoko na Mahusiano wa UTT AMIS, Bw. Daudi Mbaga, akifafanua kuhusu huduma za UTT kwa ujumla na faida zinazopatikana kwenye uwekezaji, walipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika Uwanja wa John Mwakangale, jijini Mbeya.