Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

" Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Simamieni Vizuri Miradi ya Maendeleo " Kakunda
Oct 08, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36492" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Joseph Kakunda akizungumza na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri wanaoshiriki katika semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi leo Jijini Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

 Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashuri kote nchini wameaswa kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayolenga  kuwaletea maendeleo wananchi hasa ile  inayogusa  sekta za Kilimo, mifugo, uvuvi, umeme, maji na elimu, afya, madini, na maliasili.

Akizungumza wakati akifungua semina kwa  viongozi hao inayofanyika Jijini Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) mhe. Joseph Kakunda amesema kuwa miradi  inayotekelzwa katika sekta hizo inaboresha hali za maisha ya wananchi hasa wanyonge.

" Washughulikieni wezi na wabadhirifu wa mali za umma kwani wanakwamisha miradi ya maendeleo katika maeneo yenu, tekelezeni hili kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zilizopo ili dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi itime kwa wakati" alisisitiza Kakunda.

Akifafanua, Naibu Waziri Kakunda amesema kuwa katika kuwainua wananchi kila kiongozi katika eneo lake ana jukumu la kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo zinatumika kikamilifu katika kuwaletea wananchi maendeleo na sio vinginevyo.

Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Joseph Kakunda  akiwa kwenye picha ya pamoja na  wakuu wa Wilaya wanaoshiriki katika semina ya kuwajengea uwezo leo Jijini Dodoma ambapo semina hiyo inashirikisha Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri walioteuliwa  hivi karibuni.

Mbali na kusimamia fedha zinazotolewa na serikali mheshimiwa Kakunda amwewataka viongozi hao kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo wenyeviti na maafisa watendaji wa viijiji ili kila mmoja atimize wajibu wake wa kuitisha mikutano ya kisheria inayohusu mipango na miradi ya maendeleo pamoja na kuwapatia mrejesho kupitia katika vikao halali.

"Wananchi wakichangishwa fedha kujenga madarasa, vyoo, nyumba za walimu, zahanati lazima wapewe mrejsho sahihi wa namna fedha zao zilivyotumika"; Alisisitiza Kakunda

Aliongeza kuwa miongoni mwa vigezo vinavyotumika  kupima tija ya utendaji kwenye  Halmashuri ni uwezo wa kukamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa hasa kwa miradi ambayo inapata fedha kamili kabla haijaanza mfano ujenzi wa vituo vya afya.

Lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo watendaji hao katika kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu ili kuongeza tija katika maeneo wanayosimamia kwa kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Baadhi ya mada zitakazowasilishwa ni pamoja na majukumu na mipaka ya kazi, uongozi, hisia na mahusiano mahali pa kazi zikilenga kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, muundo wa Serikali na jinsi Serikali inavyofanya kazi.

Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI  Dkt. Zainab Chaula akieleza umuhimu wa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutatua kero za wananchi katika maeneo yao pasipo kusubiri viongozi wa kitaifa kufika katika maeneo yao ili kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.

Kaimu  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo  wakati wa hafla ya kufungua semina kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri leo Jijini Dodoma.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Joseph Kakunda  akiwa kwenye  picha ya pamoja na sehemu ya wakurugenzi watendaji wa Halmashauri wanaoshiriki katika semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI)  kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi leo Jijini Dodoma.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Joseph Kakunda  akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa mada akiwemo Katibu Tawala mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini na watendaji wa Taasisi ya Uongozi mara baada ya hafla ya kufungua semina kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri  walioteuliwa kushika nyadhifa hizo hivi karibuni  ikilenga kuwajengea uwezo  leo Jijini Dodoma.

[caption id="attachment_36496" align="aligncenter" width="832"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akizungumza wakati wa semina kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri walioteuliwa kushika nyadhifa hizo hivi karibuni leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_36499" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wakifuatilia ufunguzi wa semina kwa watendaji hao leo Jijini Dodoma ikilenga kuwajengea uwezo katika kuongeza tija katika huduma wanazotoa kwa wananchi.[/caption] [caption id="attachment_36500" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akifurahia jambo na mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Mhe. Jerry Muro leo Jijini Dodoma kabla ya kuanza kwa semina kwa watendaji hao pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Halmashuri ikilenga kuwajengea uwezo katika kuongeza tija katika huduma wanazotoa kwa wananchi.[/caption] [caption id="attachment_36501" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Beatrice Kilometa akizungumza wakati wa semina kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri leo Jijini Dodoma.
                                                                                    (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi