Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakaguzi wa Kemikali Watakiwa Kuboresha Utendaji
Jun 29, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53646" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Wakaguzi hao ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kukamilika tarehe 28 Juni, 2020 katika ukumbi wa NSSF, Ilala, Dar es Salaam.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amewataka wakaguzi wa kemikali kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusiana na changamoto za ujazaji wa fomu za maombi ya usajili wa wadau wa kemikali.

Agizo hilo limetolewa jana na Dkt. Mafumiko wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Wakaguzi hao uliofanyika katika Ukumbi wa NSSF, Ilala, Dar es Salaam.

“Mkatekeleze maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu ujazaji wa fomu za taarifa za wadau wa kemikali, maoni na alama walizopata kwa ajili ya kukidhi vigezo vya kusajiliwa, zoezi hili linapaswa kuboreshwa kuanzia kwa mkaguzi, msimamizi na Mameneja wanaohusika na usajili”, alisema Dkt. Mafumiko.

[caption id="attachment_53645" align="aligncenter" width="750"] Wakaguzi wa Kemikali wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wakaguzi kutoka kwenye ofisi za Kanda kwa lengo la kuboresha shughuli za ukaguzi kwa mwaka ujao wa fedha 2020/2021. Mkutano huo umekamilika tarehe 28 Juni, 2020 katika ukumbi wa NSSF, Ilala, Dar es Salaam.[/caption]

Mkemia Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa, hilo ni eneo ambalo linahitaji kutiliwa mkazo na kujengeana uwezo zaidi ili kuweza kuboresha utendaji kazi wenu, Bodi inawapongeza kwa hatua mliyofikia, mtazamo wa Bodi ni chanya hivyo wanapaswa kupokea kwa mtazamo chanya kwa sababu lengo ni kuboresha utendaji.

Amefafanua kuwa, changamoto za usafiri na makazi kwa wakaguzi wa mipakani zinaendelea kufanyiwa kazi ambapo ile mipaka iliyoonekana na changamoto ya zaidii imepatiwa pikipiki na changamoto nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi kulingana na taratibu za Serikali.

Dkt. Mafumiko ametoa rai kwa wakaguzi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kila mmoja atimize jukumu lake na kama kuna changamoto wawasiliane na uongozi husika ili kupata ufumbuzi.

[caption id="attachment_53648" align="aligncenter" width="750"] Makaguzi wa Kemikali,  Hamisi Lugundi akichangia hoja wakati wa mkutano wa mwaka wa Wakaguzi hao uliokamilika tarehe 28 Juni, 2020 katika Ukumbi wa NSSF, Ilala, Dar es Salaam.[/caption]

Mkemia Mkuu wa Serikali amewataka wakaguzi hao kuimarisha mahusiano na wadau wanapotekeleza majukumu yao ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma kwa wateja.

“Mnapaswa kuzingatia na kuimarisha mahusiano na wadau. Kutekeleza Sheria haimaanishi kutumia ubabe au lugha isiyo rafiki, tutekeleze Sheria lakini tutumie busara na akili za ziada ili kazi ziende na kila mmoja ajiongeze na afanye inavyotakiwa” aliongeza..

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali amewaeleza Wakaguzi hao kwenda kuyafanyia kazi yaliyojadiliwa ili mkutano wa mwakani uoneshe tija kwa yale yote ambayo wamekubaliana kwenda kuyatekeleza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakaguzi hao, Afisa kutoka ofisi ya Kanda ya Kati, Revocatus Mwamba, alishukuru kwa ushirikiano unaotolewa na menejimenti katika kuwezesha kutekeleza majukumu ya mamlaka kwa ufanisi na aliomba ushirikiano huo uendelee kwa lengo la kutimiza matakwa ya Serikali na taasisi kwa ujumla.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi