Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wajawazito Longido Kupatiwa Elimu ya Afya
Aug 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Prisca  Libaga-MAELEZO, Arusha 

Wilaya ya Longido mkoani Arusha, imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuweza kutumia zahanati na vituo vya afya vilivyopo kwa ajili ya kupata matibabu yenye uhakika na hivyo kuacha matumizi ya dawa za asili ambazo hazina vipimo .

Hayo yameelezwa jana  na Mkuu wa wilaya ya Longido, Godferey Chongolo, alipokuwa akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla na kusisitiza kuwa mkakati uliopo ni kuendelea kuwahamasisha wananchi watumie hospitali kwa ajili ya afya zao .

Amesema wilaya pia inaendelea kuhamasisha wajawazito kwenda kwenye zahanati na vituo vya afya ili kwa ajili ya kujifungua kwani watakutana na wataalam wa afya ya uzazi na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kujifungua salama.

Alisema bado kuna idadi ndogo ya wakina mama wanaojifungulia katika zahanati na vituo vya afya ikilinganishwa na idadi ya watu wa Longido na kwamba wengi bado wanawatumia Wakunga wa Jadi wakati wa kujifungua.

Chongolo,amesema hamasa hiyo imewezesha kuongeza kiwango cha wajawazito kujifungulia zahanati na vituo vya afya kutoka asilimia 16 % miaka mitatu iliyopita hadi kufikia asilimia 25%

Alisema kuwa wilaya ya Longido ina vituo vya afya vitano na zahanati 23 na mkakati uliopo ni kila kata kuwa na zahanati  na kila tarafa iwe na kituo cha afya

Chongolo,alisema mkakati mwingine unaoendelea ni kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa matibabu wa CHF, ambapo idadi ya wananchi waliokwisha jiunga na CHF  imeongezeka kutoka asilimia 18% hadi asilimia 40 na katika kipindi cha miezi miwili ijayo idadi hiyo itaongezeka hadi kufikia asilimia 70%

Kuhusu dawa za magonjwa mbalimbali, mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa wilaya hiyo ina asilimia 95% ya dawa za magonjwa mbalimbali tatizo ni idadi ndogo ya wahitaji kwa sababu wengi bado wanatumia dawa za kiasili.

Amesema wilaya hiyo haina changamnoto ya upunfugu wa dawa bali changamoto iliyopo ni wananchi kufika zahanati na vituo vya afya ili dawa hizo ziweze kuwaponyesha magonjwa yanayowakabili.

Ameongeza kuwa wilaya hiyo inao upungufu wa wataalamu  wa Idara ya afya ,hivyo akamuomba Naibu waziri kuongeza ikama ya watumishi wa afya wilayani humo ili kuborehuduma ya afya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi