Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wahasibu, Waweka Hazina Watakiwa Kutumia TEHAMA Kusimamia Fedha za Maendeleo
Jun 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili kwa waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe , Katavi na Mbeya wakati akifungua awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Na: Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya

Serikali imewaagiza Wahasibu na Waweka Hazina kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao kote nchini kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) iliyopo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TEHEMA kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Bw. Erick Kitali, wakati akifungua awamu ya pili ya mafunzo ya siku nne kuhusu matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya. Mafunzo hayo yanafanyika jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuimarisha mifumo ili kuongeza tija katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.

“Kama mweka hazina au mhasibu lazima uwe mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kila eneo ambalo kuna fedha za Serikali mnazisimamia kikamilifu kwakuwa hakuna atakayevumiliwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake vyema kwa kutumia mifumo hii ambayo imeimarishwa kwa maslahi ya Taifa,” alisisitiza Kitali.

Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka mradi wa uimarishaji mifumo katika sekta za umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo ya awali kuhusu faida za mifumo mbalimbali iliyojengwa na Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na PS3 ili kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi katika mamlaka za Serikali za Mitaa, mafunzo hayo waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe ,  Katavi na Mbeya wakati wa hafla ya kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Mfumo wa Epicor 10.2 uko chini ya  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), na umejengwa kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).  Mradi huu wa miaka mitano unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

Akifafanua, Bw. Kitali amesema kuwa washiriki  wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa la kuelewa matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kwa ufasaha katika kipindi chote cha mafunzo, ili kuepuka kutekeleza majukumu yao kinyume na taratibu za mifumo hii ambayo kwa sasa imeunganishwa na kuweza kuongea ili kurahisisha utendaji na kuchochea maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka Mradi wa PS3, Bw. Desderi Wengaa, amesema kuwa OR-TAMISEMI imekuwa ikifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na mradi huo katika kuimarisha mifumo ikiwemo wa Epicor 10.2.

Aliongeza kuwa mifumo yote sasa imeunganishwa hadi ngazi ya watoa huduma, hali inayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na hivyo kusaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji  katika ngazi za vituo vya kutolea huduma.

Sehemu ya waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe ,  Katavi na Mbeya wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali wakati wa hafla ya kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma Bw. Onesmo Raphael ambaye alikuwa Mwenyekiti wa  mafunzo ya siku nne kuhusu matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2  kwa waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe ,  Katavi na Mbeya akimkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo yanafanyika jijini Mbeya.

Kutokana na kuimarishwa kwa mifumo hiyo, Serikali imeweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na huduma zinazotolewa kwa wananchi katika vituo vya kutolea huduma zikiwemo za afya na elimu.

Akizungumzia lengo la mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2, Bw. Wengaa alieleza kwamba ni kuwajengea uwezo wahasibu na waweka hazina kusimamia rasilimali fedha kikamilifu katika maeneo yao ili dhamira ya Serikali kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma bora itimie.

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa PS3, yameingia katika awamu ya tatu wiki hii, baada ya awamu ya kwanza na ya pili kufanyika wiki iliyopita.  Licha ya Mbeya, mfunzo kama haya yanayohusisha washiriki kutoka nchi nzima yanaendelea pia katika vituo vingine, ambavyo ni mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Mtwara na Kagera.

 Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali (kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka mradi wa uimarishaji mifumo katika sekta za umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa mara baada ya hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa  waweka hazina na wahasibu wa mikoa ya Njombe, Songwe ,  Katavi , awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo ya wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi, awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo kama wanavyoonekana katika picha.

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza jambo kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya, awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

Mweka hazina wa halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw. Mabula Mponeja akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi, awamu ya pili ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanafanyika jijini Mbeya.

 

(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi