[caption id="attachment_23043" align="aligncenter" width="750"] Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam .[/caption]
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa wote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.
Hayo yamesemwa leo wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.
“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka vituo vya Afya vya Serikali 524 viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya 265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.
[caption id="attachment_23044" align="aligncenter" width="768"] Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam .[/caption] [caption id="attachment_23045" align="aligncenter" width="1018"] Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.[/caption] [caption id="attachment_23046" align="aligncenter" width="750"] Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.[/caption] [caption id="attachment_23047" align="aligncenter" width="750"] Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya afya,Jhpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .[/caption]Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343 hadi kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.
“Mbali na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran.