Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wafanyabiashara Kanda ya Ziwa Watakiwa Kuzalisha Zaidi
Jun 02, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_52901" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akifafanua wakati wa mkutano wa siku moja uliowakutanisha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara kuweka mikakati endelevu ya usafirishaji wa minofu ya samaki wanaosafirisha nje ya nchi, jijini Mwanza.[/caption]

Na WUUM

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wafanyabiashara wa ukanda wa Ziwa Victoria kuongeza uzalishaji wa bidhaa za samaki, matunda, nyama na mbogamboga ili kuwezesha uwepo wa safari za uhakika za ratiba kwa mashirika ya ndege kutoka nje ya nchi kupitia mkoa wa Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kufungua kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Mifugo na Uvuvi, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera na taasisi ambazo zinashughulika na usafirishaji mkoani Mwanza amesema uwepo wa ndege za ratiba unategemea idadi ya mizigo inayozalishwa katika ukanda huo.

“Mpaka sasa kuna mashirika mawili tu ya ndege yanayosafirisha mizigo ya samaki kupeleka nje ya nchi, idadi ya ndege hizo inaweza kuongezeka tu endapo mzigo unaozalishwa utaongezeka” alisema Waziri Mhandisi Kamwelwe.

[caption id="attachment_52903" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu (Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho (kushoto), akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah na Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, wakati viongozi hao walipotembelea jengo la kuhifadhi mizigo katika kiwanja cha ndege mkoani Mwanza.[/caption]

Waziri Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa kwa sasa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) liko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kupata cheti kitakachoruhusu kusafirisha abiria na mizigo kwa nchi za (Europe hii kiswahili ni nn).

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina amewahakikishia wafanyabiashara kuwa yale ambayo yanaihusu Wizara hiyo wataanza kuyasimamia mara moja ili kuhakikisha mizigo yote inayotoka kwenye viwanda inasafirishwa kwa wakati na kuwafikia walaji.

Waziri Mpina ameongeza kuwa mpaka sasa kuna zaidi ya tani 200 za samaki ambazo huzalishwa kila siku kupitia viwanda vya Mwanza kuiomba Wizara kuhakikisha ratiba za ndege zinaongezeka ili kuwafanya wafanyabiashara kuzalisha zaidi.

[caption id="attachment_52902" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AirCO, Kumar Bharat akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu (Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye tai ya bluu), Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kushoto), wakati viongozi hao walipotembelea jengo la mizigo katika kiwanja cha ndege mkoani Mwanza.[/caption]

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amemshukuru Waziri Mhandisi Kamwelwe kwa kuzikutanisha sekta zote ili kujadili na kuja na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha usafirishaji wa samaki unaendelea na kuwa na manufaa kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya Ziwa.

Waziri Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara kuwa wataendelea kusimamia ubora wa biadhaa hizo kwa kuboresha muonekano wa vifungashio ili uweze kulingana na mahitaji ya soko.

Mashirika ya Ndege ya Rwanda na Ethiopia yalianza rasmi kusafirisha minofu ya samaki na mabondo tarehe 12 Mei 2020 ambapo mpaka sasa Shirika la Ndege la Rwanda limeshafanya safari mbili na Shirika la Ndege la Ethiopia limeshafanya safari moja na makampuni hayo kwa pamoja yameweza kusafirisha jumla ya tani 68.2.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi