Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau wa Maendeleo Waaswa Kuchangia Sekta ya Elimu
Oct 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_17224" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel akimuelekeza Katibu msaidizi wa Tume hiyo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Bw. Antony Damiano namna ya kutumia mfumo rasmi wa mawasiliano serikalini kwa njia ya mtandao, mapema leo katika Ofisi za Tume hiyo Wilayani humo.

[/caption] [caption id="attachment_17230" align="aligncenter" width="876"] Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bahi Bw. Patrick Gwivaha akizungumza na wajumbe kutoka Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) walioongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi Devotha Gabriel.[/caption]

Frank Mvungi- Maelezo – Dodoma

Wadau wa maendeleo wametakiwa kujitokeza kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuongeza tija na kuchochea kasi ya maendeleo ya sekta hiyo na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika mahojiano maalum Wilayani Bahi Mkoani Dodoma Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel amesema kuwa Tume hiyo imejipanga kutatua changamoto zinazowakabili walimu hapa nchini kwa kujenga mifumo rafiki ya TEHAMA ukiwemo ule utakoondoa matumizi ya karatasi katika shughuli za kila siku za Tume hiyo (Paperless system).

[caption id="attachment_17231" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel akikabidhi moja ya vitendea kazi wakati wa ziara yakutembelea Ofisi za Tume hiyo Wilayani Bahi mapema leo.[/caption]

“Takribani asilimia sitini ya watumishi wa Serikali ni walimu hivyo ni muhimu kwa wadau kujitokeza na kuunga mkono juhudi za Tume katika kujenga mifumo  hii ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uendeshaji na kuboresha huduma katika ofisi zetu hasa ngazi ya Wilaya.” Alisisitiza Devota.

Akifafanua Bibi Devota amesema kuwa Tume hiyo imejipanga vyema kuhakikisha kuwa mifumo itakayojengwa inakuwa rafiki na inasaidia kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa kwa Tume hiyo.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Wilaya ya Bahi Bw. Antony Damiano amesema kuwa kuwepo kwa Tume ni ukombozi mkubwa kwa walimu hapa nchini kwani changamoto zilizokuwa zikiwakabili walimu kama vile kuchelewa kupandishwa madaraja, kuthibitishwa kazini,Kustaafu na kupatiwa barua za ajira sasa zimepatiwa ufumbuzi mara baada ya Tume hiyo kuanzishwa.

Kwa sasa huduma zimesogezwa karibu zaidi na walimu hali inayochochea kuongezeka kwa kiwango cha uzingatiaji wa maadili, sheria na Taratibu za kazi katika Wilaya ya Bahi.

“Tunapa fursa ya kusisitiza maadili kwa kuwa sasa tunawatembelea walimu katika maeneo yao ya kazi na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kutafuta ufumbuzi” Alisisitiza Damiano

Pia Damiano alitoa wito kwa Walimu kuzingatia maadili na kujitoa kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao hali itakayosaidia kukuza sekta ya elimu hapa nchini.

Tume ya utumishi wa Walimu imeanzishwa kwa sheria namba 25 ya mwaka 2015 na imefanikiwa kuanza kutatua changamoto zinazowakabili walimu hapa nchini kwanza kwa kuanzisha Ofisi kila Wilaya ili kusogeza huduma zake karibu na Walimu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi