Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau wa Elimu Changamani Baada ya Msingi (IPPE) Watakiwa Kuboresha Elimu Kukuza Kizazi Chenye Ujuzi.
Nov 21, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_38619" align="aligncenter" width="800"] Kaimu  Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt Honest Kapasika akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya wadau wa elimu changamani baada ya Msingi (IPPE) kwa wamiliki na wasimamizi wa shule huria leo Jijini Dodoma.[/caption]  

Na Daudi Manongi-MAELEZO

Wadau wa Elimu Changamani baada ya msingi (IPPE) nchini wametakiwa  kubuni mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuboresha elimu katika shule zao na kusaidia kujenga kizazi chenye ujuzi,weledi na maarifa ya kupambana na changamoto mbalimbali za maendeleo zinazokabili jamii yetu kwa sasa.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu  Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt Honest Kapasika wa  Taasisi ya Elimu ya Watu wazima(TEWW) nchini wakati akifungua Semina ya siku moja kwa wadau hao leo Jijini Dodoma.

"Semina hii imekuja katika wakati muafaka, ni matumaini yangu kuwa mwisho wa semina hii mtajiwekea maazimio  ambayo kila mmoja anapaswa kufuata",Aliongeza Dkt Kapasika.

Aidha Dkt Kapasika ameeleza kuwa semina hiyo itajikita katika maeneo makuu manne ambayo  ni Kukuza uelewa wa taratibu mbalimbali za uendeshaji wa shule huria zenye programu za mpango wa elimu changania baada ya msingi,

 Pili zitachambua changamoto  mbalimbali zinazikabili utoaji wa mpango elimu changamani baada ya msingi ,

Tatu itasaidi  kukuza uwezo wa wadau wa mpango wa elimu changamani bada ya msingi kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa mtaala wa elimu nje ya mfumo rasmi pamoja na elimu changamani baada ya msingi ,

Nne  itakuza uelewa wa mfumo wa upimaji na kutunuku vyeti kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi na mpango wa elimu changamani baad aya msingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa (TEWW) , Baraka Kionywaki amesema  kuwa lengo hasa la semina hiyo ni kuhakikisha kuwa programu hizo zinatolewa katika ubora ambao Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inauhitaji na pia TEWW imeanza kufungia vituo ambavyo vinakiuka programu izo kwa kutoa programu zinazotolewa katika mfumo rasmi.

Nae Sister Erneta Mlelwa kutoka Chuo cha Ufundi Mariele  Namanga amesema kuwa watapokea maelekezo watakayopewa na TEWW ili kuboresha elimu na kukuza kiwango cha ufaulu katika vituo vyao kama inavyotakiwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi