Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watafiti Sekta Isiyo Rasmi Watakiwa Kuongeza Weledi
Apr 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="900"] Mratibu wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Bibi Ened Munthali akifungua mafunzo ya wadadisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi Tanzania hawapo (pichani) leo mjini Dodoma.[/caption]   [caption id="attachment_30166" align="aligncenter" width="831"] Mratibu wa MKURABITA Bibi Serapia Mgembe akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa utafiti wa sekta isiyo rasmi Tanzania utakaofanyika Tanzania Bara na Visiwani wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi Tanzania hawapo (pichani) leo mjini Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma

Wadadisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi Tanzania wametakiwa kutekelza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia sheria ili kuepuka mkono wa sheria pale ambapo watakwenda kinyume na taratibu za utafiti huo. kwa kuwa unalenga  kusaidia katika kukuza uchumi .

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na  Mratibu wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Bibi. Ened  Munthali wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wadadisi ili waweze kutekeleza jukumu la kukusanya taarifa katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kuhusu sekta isiyo rasmi.

Akifafanua  Bibi. Munthali amesema, Serikali imeagiza MKURABITA kufanya utafiti huo ili kuiwezesha Serikali  kupanga mipango ya maendeleo katika ngazi ya mikoa kwa kuzingatia matokeo ya utafiti huo na kutolewa kwa ngazi ya mkoa husika na  ngazi ya Taifa.

[caption id="attachment_30167" align="aligncenter" width="843"] Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ( NBS) Bw. Ephraim Kwesikwabo akiwaasa wadadisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi Tanzania hawapo (pichani) leo mjini Dodoma kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka mkono wa sheria kwa wale watakokwenda kinyume cha maadili ya jukumu la kukusanya taarifa sahihi katika mikoa waliyopangiwa.[/caption]

" Naomba muwe makini katika kukusanya taarifa za utafiti huu kwa kujiepusha na vitendo vya uchakachuaji wa taarifa wakati mtakapokuwa katika mikoa mliyopangiwa kukusanya takwimu ili kufanikisha utafiti huu kwa wakati na kuleta matokeo tarajiwa " Alisisitiza  Munthali.

Aliongeza kuwa  Serikali ya Awamu ya Tano inayo dhamira ya dhati yakupeleka maendeleo hasa ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa wananchi hivyo utafiti huo utakapokamilika utasaidia Serikali katika ngazi ya mikoa kupanga mipango ya maendeleo  kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi.

Kwa upande wake Mratibu wa MKURABITA  Bibi. Serapia Mgembe amesema kuwa wadadisi hao wanamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa kutokana na jukumu walilokabidhiwa la kukusanya taarifa zitakazoisaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa ufanisi.

" Wote mtakaoshiriki katika utafiti huo ni vyema mkatambua kuwa mmepewa jukumu hili na Serikali hivyo ni dhamana kubwa mliyokabidhiwa mnayopaswa kuitunza kwa kufanya kazi hii kwa weledi na ustadi ili  lengo la utafiti lifikiwe " Alisisitiza Mgembe

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ( NBS) Bw. Ephraim  Kwesikwabo amesema kuwa matokeo ya utafiti huo yatatoa mwelekeo mpya wa sera mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali kwa ajili yakuwawezesha wananchi kumiliki biashara na rasilimali katika mfumo rasmi hali itakayosaidia kuongeza  kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi mmoja mmoja na kupanua wigo wa ukusanyaji mapato .

Aidha Kwesigabo alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa  Ofisi za Taifa za Takwimu(NBS) katika mikoa wakati wa ukusanyaji  wa takwimu za utafiti wa sekta isiyo rasmi.

[caption id="attachment_30168" align="aligncenter" width="772"] Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya wadadisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi Tanzania leo mjini Dodoma.[/caption]

Ushirikiano wa wananchi ni nguzo muhimu katika upatikanaji wa takwimu bora zitakazosaidia uapangaji wa mipango na ufanyaji wa maamuzi katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Utafiti huo unafanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya mtakwimu Mkuu Zanzibar na utasaidia katika uboreshaji wa umiliki wa biashara na rasilimali kwa wananchi wanyonge nchini, mafunzo kwa watafiti hao yameanza Aprili 6, 2018 na kutarajiwa kukamilika Aprili 12, 2018.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi