Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Black Engineering kutoka nchini Italia Massimo Fogliati ambao ndio walioandaa sherehe za Ufunguzi wa African Football League Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Oktoba 21, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Waziri amewashukuru kwa kufanikisha ufunguzi huo, pamoja na kutoa ajira na fursa kwa Watanzania ambao walihusika katika ufunguzi huo.
Mhe. Dkt. Ndumbaro amewakaribisha wawekezaji hao kufungua tawi hapa nchini kwakua tayari wana matawi Saud Arabia na Dubai.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji huyo, Bw. Massimo amepokea pongezi hizo na kushukuru Serikali na Wadau wote wa michezo kwa ushirikiano, ambapo ameahidi kurudi nchini kwa ajili ya kutafuta fursa zaidi na uwekezaji.