Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vyombo vya Habari Vyaaswa Kuzingatia Maadili.
Jan 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27251" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaeleza watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) umuhimu wa kubeba ajenda ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda wakati wa ziara yakutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma iliyoanza mapema leo.

[/caption] [caption id="attachment_27257" align="aligncenter" width="1000"] Muwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Mkoani Dodoma Bw.Felix Mushi akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika Ofisi za Kampuni hiyo Mkoani Dodoma.[/caption]

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Akiwa katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Abbasi amevitaka vyombo vya habari vya Dodoma kuwa tayari na ujio wa Serikali kuhamia Dodona kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani humo.

AA

"Kwa baadhi ya matukio yaliyofanyika hapa Dodoma nimeona uzubaifu kwa baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahabari wenzangu tuchangamke kwani matukio mengi ya Serikali yatafanyika hapa" amefafanua Dkt. Abbasi.

[caption id="attachment_27259" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Mkoa wa Dodoma mara baada ya kutembelea Ofisi hizo mapema leo ili kujionea utendaji wa Kampuni hiyo na Kusisitiza uzingatiaji wa maadili ya uandishi wa habari.
[/caption] [caption id="attachment_27253" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiagana na watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Mkoani Dodoma mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Kampuni hiyo mapema leo.[/caption]

Aidha, Dkt. Abbasi ameutaka uongozi wa TSN kufuata maadili katika utendaji kazi kwani wananchi hutazama kampuni hiyo kwa jicho la utofauti kama chombo cha Serikali.

“Mkiwa kama Kampuni ya Magazeti ya Serikali mnatakiwa kuibeba agenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda" ameongeza Dkt.Abbasi.

Akiwa katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd mkoani humo, Dkt Abbasi amesema kuwa asilimia 99 ya waandishi wamejikita katika masuala ya kisiasa kuliko masuala ya maendeleo ya nchi au bajeti mbalimbali zinazohusu serikali hivyo ameshauri vyombo vya habari kujikita katika zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya jamii.

Aidha, Dkt. Abbasi amesisitiza umuhimu wa wanataaluma ya habari kujiendeleza kitaaluma ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, mwandishi wa habari atatakiwa kuwa na  atashahada ya taaluma ya uandishi wa habari.

[caption id="attachment_27254" align="aligncenter" width="1000"] Watumishi wa Gazeti la Mwananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma iliyoanza Januari 17, 2017.
[/caption] [caption id="attachment_27255" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiagana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Mkoani Dodoma mara baada ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo na kuzungumza na wafanyakazi, kushoto ni Mkuu wa Kanda wa Gazeti la Mwananchi. (Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma).[/caption]

Akizungumzia kuhusu upatkanaji wa habari, Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imewekeka mfumo wa kisheria kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kutoka katika Wizara na Taasisi zake.

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesisitiza waandishi wa habari kujisajili ili wapatiwe vitambulisho (Press Card) kwani kuanzia mwezi Machi mwaka huu katika matukio yote ya viongozi wakuu wa Kitaifa,  kila mwanahabari atatakiwa kuwa na kitambulisho hicho.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi