Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vyombo Vya Habari Vyaaswa Kuripoti Miradi na Programu Zinazotekelezwa na SADC
Nov 30, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Frank Mvungi - Botswana

Waratibu wa vyombo vya Habari wa nchi Wanachama  wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)  wametakiwa  kuhamasisha vyombo vya habari katika  nchi wanachama kuripoti habari za miradi na progamu zinazotekelezwa na umoja huo kwa manufaa ya wananchi wa nchi wanachama.

 Akizungumza katika  hafla ya ufunguzi  kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax , inayofanyika  Makao Makuu ya Umoja huo mjini Gaborone nchini Botswana , Mkuu wa  mawasiliano wa Jumuiya hiyo Bi Barbara  Lopi amesema Warsha hiyo itawajengea uwezo waratibu hao ili waweze kutekeleza jukumu la kuhamasisha vyombo vya habari kutangaza umuhimu wananchi kutumia fursa zilizopo katika nchi wanachama kuchochea maendeleo na Ustawi wa umoja huo.

[caption id="attachment_23803" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba ya Ufunguzi wa Warsha ya Waratibu wa Vyombo vya Habari katika nchi wanachama wa SADC yanayofanyika Mjini Gaborone nchini Botswana.[/caption] [caption id="attachment_23804" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa Shiriki wa Warsha hiyo kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Warsha hiyo inayofanyika (Makao Makuu ya SADC)

[/caption]

“ Warsha hii ni Fursa kwa waratibu wa vyombo vya habari wa nchi Wanachama kujengewa uwezo wa namna bora yakushirikiana na vyombo vya habari  katika kutangaza  miradi  yanayotekelezwa na SADC kwa manufaa ya nchi wanachama hasa  masuala yanayochochea ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama ”  Alisisitiza Lopi

Warsha hiyo ya siku tatu  inawashirikisha waratibu  kutoka nchi wanachama wa SADC  wenye jukumu lakuhakikisha kuwa  umoja huo unatangazwa na kuwanufaisha wananchi wote katika nchi wanachama ili waweze kutekeleza vipaumbe vya umoja huo ikiwemo uimarishaji wa viwanda vitakavyosaidia kuzalisha ajira.

Baadhi ya mada zitakazowasilishwa katika warsha hiyo ni pamoja na Muundo wa Jumuiya hiyo,Umuhimu na Majukumu ya Waratibu wa Vyombo vya Habari kwa kila nchi.

[caption id="attachment_23807" align="aligncenter" width="682"] Mkuu wa Mawasiliano wa SADC bi Barbara Lopi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stagomena Tax, Warsha hiyo inalenga kuwajengea uwezo Waratibu wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) kutoka nchi wanachama wa SADC inafanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Mjini Gaborone nchini Botswana kwa siku tatu.( Picha na SADC )[/caption]

Kwa upande wake Muwakilishi wa Shirika la Maendeo la Ujerumani Bw. Felix  Reimer amesema kuwa Shirika lake limekuwa likifanya kazi na SADC kupitia Kitengo cha Uhusinao ili kufanikisha masuala mbalimbali ya Mawasiliano ikiwemo kujenga uwezo kwa waandishi wa Habari wan chi wanachama ili waweze kuripoti habari zinazohusu SADC.

Aliongeza  kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa Shirika hilo kuendelea kushirikiana na  SADC kwa kuwa umoja huo una umuhimu mkubwa katika kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kuwa ni kupitia imoja huo nchi wanachama zinaweza kushirikiana na kutekeleza mipango ya maendeleo.

SADC inaendesha warsha yakuwajengea uwezo waratibu wa vyombo vya Habari kwa nchi wanachama ili kujenga uwezo wa kuwashirikisha wananchi katika masuala yote yanayohu SADC zikiwemo fursa zilizopo na kwa nchi wanachama.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi