Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vyombo vya Habari ni Mwalimu - Waziri Mwakyembe
Nov 05, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_48626" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe akifungua mkutano wa wadau wa habari jijini Arusha unaouhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.[/caption]

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha

Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na mashirika mengine katika kukabiliana na kutatua changamoto zozote hasi ambayo zinazotishia uhai na usalama wa waandishi wa habari na wafanyikazi wengine katika vyombo vyote vya habari vikiwemo vya mtandaoni.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa wadau wa habari kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.

“Vyombo vya habari ni mwalimu. Sisi kama Serikali tunaona umuhimu mkubwa sana wa vyombo vya habari, chombo cha habari kinatuwezesha dunia nzima kujua tunasema nini na ujumbe wetu unataka nini. Vyombo vyetu vya habari ni lazima vitambue vinawajibu wa kuleta heshima katika tasnia ya habari na kumpa ulinzi mwanahabari” alisema Waziri Dkt. Mwakyembe.

[caption id="attachment_48625" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati ufunguzi wa mkutano wa wadau wa habari jijini Arusha kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Tirso Dos Santos (kushoto).[/caption]

Katika kusimamia usalama wa mwanahabari, Waziri Dkt. Mwakyembe amesema kuwa vyombo vya habari vinawajibu mkubwa wa kuhakikisha maisha ya mwanahabari yapo salama na kusisitiza kuwa usalama wa wanataaluma hao unaanzia chumba cha habari.

Waziri Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 inatambua uandishi wa habari ni taaluma kamili ikiwa ikisimamia na kuweka masharti ya kukuza na kuimarisha taaluma na weledi katika tasnia ya habari. Sheria hiyo imeweka Bodi ya Ithibati ya Wanahabari, Baraza Huru la Habari, kuweka  mfumo wa usimamizi wa huduma za habari, Mfuko wa wanahabari pamoja na kuhakikisha wananahabari wanakuwa na bima wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

“Vyombo vya habari vyenyewe ni lazima vitambue vina wajibu mkubwa wa kuhakikisha maisha ya wanahabari yapo salama, usalama unaanzia chumba cha habari. Usalama wa kwanza ni maisha ya mwanahabari mwenyewe na stahili zake za kila siku ikiwemo mshahara. Hiki suala nimelisema mara kwa mara, tutaanza kulazimishana kwa sheria. Mwanahabari hawezi kuendelea kukimbilia kwenda kwa chanzo chake cha habari kuomba bahasha iwe ndio sehemu ya haki yake, Hii ni fedheha na kuzalilisha taaluma ya habari” alisisitiza Waziri Dkt. Mwakyembe.

Akijibu moja ya maazimio ya mkutano wa mwaka 2018 linaloitaka Serikali kuunda uwezeshaji wa kisheria na wa kitaalam juu ya uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari miongoni mwa mambo mengine kukubali mamlaka ya Mahakama ya Afrika juu ya haki za binadamu na ya raia wa kawaida wakiwemo waandishi wa habari, Waziri Dkt. Mwakyembe alifafanua kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi saba za Afrika ambazo tayari zimetia saini na kuridhia mkataba huo, hivyo azimio hilo lilishafanyiwa kazi hata bila ya wadau hao wa habari kuiomba Serikali.

[caption id="attachment_48624" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Tirso Dos Santos, akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati ufunguzi wa mkutano wa wadau wa habari jijini Arusha unaouhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.[/caption]

Aidha, Waziri Dkt. Mwakyembe amewapongeza vijana Mussa Kalokola na Michael Kimollo kutoka Kampuni ya Hype Interactive Ltd ya jijini Dar es salaam kwa kwa kubuni na kutengeneza mfumo ambao ni wa kwanza kutumika duniani unaowezesha kupatikana taarifa na takwimu za wanahabari wanaopata madhila mbalimbali wanapotimiza majukumu yao.

Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Tirso Dos Santos, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, amesema kuwa uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari ni muhimu kukuza uelewa, kuelimisha watu, kukuza demokrasia hatua inayosaidia kuendeleza juhudi za kufikia lengo la maendeleo endelevu.

Akinukuu maneno ya Katibu Mkuu huyo wa UN António Guterres, Dos Santos alisema “Waandishi wa habari wanapolengwa, jamii kwa ujumla huumia nao. Bila uwezo wa kulinda waandishi wa habari, uwezo wetu wa kuendelea kuwa na habari na kuchangia utoaji wa maamuzi unazuiwa sana. Bila waandishi wa habari kuweza kufanya kazi zao kwa usalama, tunakabiliwa na matarajio ya ulimwengu wa machafuko na habari zisizo na uhakika.”

[caption id="attachment_48621" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe (hayupo pichani) wakati ufunguzi wa mkutano wa wadau wa habari jijini Arusha kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.[/caption]

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewahakikishia usalama washiriki wa mkutano huo kwa muda wote wa mkutano wao na kuwahimiza kuwa mkutano huo uwe ni dira mpya katika utendaji wao wa kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za taaluma yao.

Zaidi ya hayo Mkuu huyo wa Mkuoa amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanawajibu wa kuandika na kutangaza habari zenye ukweli na uhakika badala ya kuandika na kutangaza habari wanazozipata kupitia mitandao ya kijamii bila kufanya ufuatiliaji kupitia mtoa taarifa au ofisi husika.

[caption id="attachment_48622" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari ya UNESCO Tanzania Nancy Kaizilege akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aweze kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe wakati ufunguzi wa mkutano wa wadau wa habari jijini Arusha kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.[/caption]

Siku za kimataifa ina fursa ya kuelimisha umma juu ya maswala yanayohusu masuala ya hanbari na wanahabari, kuhamasisha utashi wa kisiasa na rasilimali katika kutatua changamoto za ulimwengu, na kuongeza mafanikio ya ubinadamu. Siku hii huadhimishwa kila mwaka Novemba 2 ambapo kwa Tanzania mkutano huo unafanyika kwa siku tano kuanzia Novemba 4 hadi 8, 2019 jijini Arusha.

[caption id="attachment_48623" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa wadau wa habari unaoendelea jijini Arusha wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaouhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.[/caption]

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi