Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Viongozi Watakiwa Kutoa Ushirikiano Kwa Wadadisi
Nov 18, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_22911" align="aligncenter" width="725"] Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifunga mafunzo ya Wadadisi , Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi mapema leo mjini Dodoma unaotarajiwa kufanyika nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja ukihusisha kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara.

[/caption] [caption id="attachment_22908" align="aligncenter" width="808"] Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akimkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kufunga mafunzo ya Wadadisi , Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi mapema leo mjini Dodoma.
[/caption] [caption id="attachment_22907" align="aligncenter" width="781"] Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi , Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti huo mapema leo mjini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi Wetu-Dodoma

Serikali imewakata Viongozi katika Ngazi ya Taifa, Mikoa, Wilaya, Halmashuri, Kata na Vijiji kote Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi nchini kutoa ushirikiano kwa Wadadisi , Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi unaotarajiwa kufanyika nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja ukihusisha kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wadadisi, Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kupata takwimu sahihi zitakazowezesha Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa kuzingatia matokeo ya utafiti huo.

“Nawaasa wote mtakaohusika katika kukusanya takwimu hizi kufanya kazi hii kwa uzalendo na moyo wa kujituma kwa kuwa Serikali inawategemea ninyi kama vijana kutoa mchango wenu utakaowezesha kufikiwa kwa maendeleo endelevu” alisisitiza Dkt. Mpango

[caption id="attachment_22913" align="aligncenter" width="700"] Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia TEHAMA bw. Baltazar Kibola akieleza mikakati ya Ofisi yake katika kusaidia kufanikisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi mjini Dodoma mapema leo.
[/caption] [caption id="attachment_22912" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb), ambaye ni mgeni rasmi mapema leo mjini Dodoma.[/caption]

Akifafanua Dkt . Mpango amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira za muda kwa vijana 620 watakaoshiri katika kukusanya takwimu za utafiti huo.

Pia alitoa wito kwa wananchi wote ambao kaya zao zimechaguliwa kushiriki katika utafiti huo kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi za kila mwanakaya mwenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea.

“Natambua kuwa suala la kukusanya takwimu rasmi za Serikali ni shirikishi hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutoa taarifa sahihi kwa lengo kusaidia Serikali kupanga mipango endelevu ya maendeleo” alisisitiza Dkt. Mpango.

Aidha Dkt. Mpango aliwashukuru wadau wa Maendeleo ambao wameshiriki kuwezesha utafiti huo kufanyika ambao ni pamoja na Benki ya Dunia, Ubalozi wa Ireland, UNICEF, WHO, UN Women.

[caption id="attachment_22910" align="aligncenter" width="655"] Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa kwenye Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wamafunzo ya Wadadisi , Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi mapema leo mjini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa aliwataka wadadisi hao kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao ili kutimiza azma ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Aliongeza kuwa jambo muhimu ni kukusanya taarifa hizo kwa usahihi na kwa wakati ili kazi hiyo ikamilike kwa muda muafaka.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundo mbinu ya TEHAMA bw. Baltazar Kibola amesema kuwa watatoa ushirikiano wakutosha kwa wadadisi hao katika ngazi zote kuanzia Mikoa, Wilaya, Halmashuri, Kata, Vijiji na Vitongoji ili  azma ya Serikali kupata takwimu sahihi itimie kama ilivyopangwa.

Serikali ya Awamu ya Tano na zilizotangulia zimeendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kupambana na umasikini tangu Tanzania ilpopata uhuru 1961 juhudi hizo zitafanikiwa kutokana na zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara 2017/18.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi