Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Viongozi Halmashauri Waaswa Kuacha Migogoro
Jul 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6200" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. George Simbachawene akifafanua jambo wakati akizungumza za viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kondoa kwenye kikao maalumu alichokiitisha kutazama chanzo cha migogoro Wilayani humo. (Picha na: OR -TAMISEMI)[/caption]

Na. Mwandishi Wetu

Viongozi katika halmashauri nchini wametakiwa kuacha migogoro isiyokuwa na tija na badala yake waungane ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI)  Mhe. George Simbachawene alipokuwa akiongea na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kondoa akiwemo Mkuu wa Wilaya, Madiwani, Mbunge, viongozi wa dini pamoja na wazee wa mji huo kwa lengo kuwasikiliza viongozi hao ili kujua nini chanzo cha migogoro ya mara kwa mara katika halmashauri ya Mji wa Kondoa.

“Wilaya yenu imekuwa ni miongoni mwa wilaya kadhaa nchini ambazo zimekuwa na tatizo la kiuongozi kitu ambacho kisababisha kusua sua kwa maendeleo katika halmashauri yenu. Kupitia kikao hiki ningependa kufahamu kutoka kwenu nini hasa sababu ya migogoro hii na kama ikiwezekana tupate suluhisho la migogoro hii ili tuendelee kufanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi,”alisema Waziri.

[caption id="attachment_6202" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Mh. Ashantu Kijaji, akizungumza katika kikao maalumu kilichoitishwa tarehe 08.07.2017 Wilayani Kondoa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. George Simbachawene, kuangazia Chanzo cha Migogoro ya kiuongozi Wilayani Kondoa.[/caption]

Miongoni mwa migogoro iliyopo ni baada ya madiwani wa halmashauri ya mji huo kumuondoa ktika uongozi Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw. Alhaji Omar Kariati ambapo baada ya kuondolewa kwa Mwenyeki huyo madiwani wamegawanyika katika makundi mawili ya wanaaounga mkono kuondolewa kwake na wale kitu kinachopunguza ufanisi katika utendaji kazi katika halmashauri hiyo.

Akichangia mada katika kikao hicho, Sheikh Twalha, sheikh mkuu wa mkoa msaafu alimshukuru Mhe. Waziri kwa kuitisha kikao hicho na kuwataka viongozi kuitisha vikao vya namna hiyo mara kwa mara ili kutatua migogoro kabla haijawa mikubwa na kuzuia maendeleo.

[caption id="attachment_6205" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. George Simbachawene (wa tatu kuanzia kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Bw. Phares Kibasa kwenye kikao maalumu alichokiitisha ili kusikiliza ni nini chanzo cha migogoro ya kiuongozi Wilayani Kondoa.[/caption] [caption id="attachment_6206" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa Wazee maarufu Wilayani Kondoa Sheikh Twalha akizungumza wakati wa kikao maalumu kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji huo kilichoitishwa tarehe 08.07.2017 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. George Simbachawene kuangazia Chanzo cha Migogoro ya kiongozi Wilayani Kondoa.[/caption]

Vile vile aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuungana na kufanya kazi kwa pamoja kwani uongozi ni dhamana hivyo kuna kila sababu ya kufanya kazi kwa pamoja.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Veneranda Makota, amewataka viongozi wa halmashauri hiyo kusameheana kwa yale yote yaliyopita na badala yake warudi kuwa kitu kimoja na kuwatumikia wananchi kwani kila mmoja yupo katika nafasi yake ili kuwatumikia wananchi.

Akifunga kikao hicho kilichodumu kwa zaidi ya saa nane Mheshimiwa Simbachawene aliwaagiza viongozi wote wa halmashauri hiyo kutambua mipaka ya kiuongozi baina yao kwani kila mmoja ana madaraka, majukumu na vilevile kila mmoja ana nafasi yake na anamuhitaji mwenzie ili kutekeleza majukumu yake kiufanisi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi