Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vijana Wakumbushwa Umuhimu wa Kulipa Kodi
Jun 17, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_3730" align="aligncenter" width="750"] Mwalimu wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana kuhusu Nguvu ya Kodi, ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA Taifa Bw. Suleiman Makwita na Muongoza mada Bi. Nuria Mshare. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.[/caption]     [caption id="attachment_3732" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Irene Kalumuna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3736" align="aligncenter" width="750"] Muongozaji wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Nuria Mshare akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA, Bw. Suleiman Makwita na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.[/caption] [caption id="attachment_3742" align="aligncenter" width="750"] Washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakichangia mada wakati wa mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid Tanzania.[/caption] [caption id="attachment_3745" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakifuatilia mada wakati wa mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid.(Picha na: Frank Shija)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi