Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Utoaji wa takwimu bora, chanzo cha matokeo chanya ya maendeleo.
Jan 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na: Mwandishi Wetu

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha tetesi kwamba sheria ya takwimu ya mwaka 2015 inazuia takwimu zinazofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini na kusema kuwa sheria hiyo haihusiki kabisa kwani vyuo vikuu wana sheria zao zinazowasimamia na kuwaongoza katika utoaji wa takwimu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alipokuwa akizungumza leo na wadau mbalimbali wa takwimu jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa  semina ya siku moja kuhusiana na uelewa wa matumizi wa sheria ya takwimu namba 9 ya mwaka 2015 iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere.

Akiendelea kuzungumza na wadau hao wa takwimu Dkt chuwa amesema kuwa ofisi ya takwimu ni tasnia kama zilivyo tasnia nyingine za kiserikali hivyo utoaji wa takwimu siyo suala jepesi kwani ni jambo linalohitaji kufuata na kuzingatia sheria katika utoaji wa takwimu hizo.

“Ofisi ya takwimu ni tasnia kama zilivyo tasnia nyingine za kiserikali kama vile asasi za kiraia na nyinginezo, hivyo utoaji wa takwimu siyo suala jepesi kwani ni jambo linalohitaji kufuata na kuzingatia sheria katika utoaji wa takwimu hizo” amesema Dkt Chuwa.

Pia amesema kuwa matumizi ya takwimu zilizo rasmi wigo wake umekuwa mpana zaidi na utoaji wa takwimu bora kunasaidia na kuleta matamanio ya kuondokana na wimbi la umaskini na kuongeza kuwa serikali inayotaka matokeo chanya katika safari ya maendeleo ni lazima kufuata takwimu zilizo bora na rasmi.

“utoaji wa takwimu bora kunasaidia na kuleta matamanio ya kuondokana na wimbi la umaskini na kuongeza kuwa serikali inayotaka matokeo chanya katika safari ya maendeleo ni lazima kufuata takwimu zilizo bora na rasmi” amesema Dkt Chuwa.

Aidha amebainisha kuwa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza baada ya kupitishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 sasa jukumu kubwa la ofisi ya takwimu ni kuratibu na kusimamia mfumo mzima wa ukusanyaji na utoaji wa takwimu zilizo bora na rasmi.

             

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi