[caption id="attachment_5394" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akiongea na Menejmenti ya Mkoa wa Songwe (hawapo pichani) alipotembelea mkoa huo jana , kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bw. Herman Paul Tesha.[/caption]
Na: Zawadi Msalla-WHUSM
Watumishi wa Mkoa wa Songwe wameshauriwa kuwa na utamduni wa kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni nyenzo muhimu ya kufikia malengo na azma iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
Hayo yamezungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati alipokutana na Sekretarieti ya Mkoa huo,na kuwaeleza kuwa ni wakati muafaka kwa watumishi kupata na kutoa elimu sahihi ya kuwafanya wananchi wapende utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii bila kulazimishwa.
[caption id="attachment_5395" align="aligncenter" width="750"]“Ni vizuri watumishi wakawa na elimu ya kutosha kuhusu utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya kiutumishi ili kuweza kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi yetu,” alisema Prof. Elisante
Prof. Elisante aliongeza kuwa ni muhimu kwa watumishi wa Umma na watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa kushirikiana ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya taifa .
[caption id="attachment_5398" align="aligncenter" width="750"]Aidha alieleza kuwa ni budi Watanzania kufuata maadili na kuzingatia muda katika utunzaji wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho kwa kuwa ni vigumu kutegemea mtu kutoka nje ya nchi kutunza rasilimali za nchi yetu.
Vilevile Prof. Elisante aliwaomba watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Songwe kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kuipeleka mbele nchi katika uchumi wa kati na kuwa Taifa la Viwanda.
[caption id="attachment_5401" align="aligncenter" width="1000"]Katika hatua nyingine Prof.Elisante aliipongeza Wilaya ya Ileje kwa kuwa mfano katika utendaji uliopelekea mafanikio makubwa kwa mkoa wa Songwe na kuzitaka Wilaya nyingine kuiga mfano huo.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa huo Bw.Herman Tesha aliahidi kutekeleza ushauri ulitolewa na Katibu Mkuu Prof.Elisante licha ya uchanga wa mkoa wake kwa kuwa anaamini mwamko na ari ya watumishi waliopo kwa pamoja wanaweza kuleta maendeleo.