Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uongozi Institute Yaandaa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi
Oct 15, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36844" align="aligncenter" width="727"] Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Issa Ngi'mba akifungua mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption]

Frank Mvungi

Maboresho yanayofanyika ndani ya Jeshi la Polisi yametajwa kuongeza tija katika huduma zinazotolewa kwa wananchi hali inayochangia kupungua kwa vitendo vya uhalifu nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Ngimba amesma mafunzo ya uongozi kwa makamanda wa polisi wa mikoa na wale wa makao makuu yatasaidia kuongeza weledi kwa watendaji hao wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka na yatasaidia kutatua changamoto zilizopo katika utendaji wenu katika mikoa mkiwa kama Makamanda wa Polisi”. Alisisitiza Ngimba.

Akifafanua, Ngimba amesema mafunzo hayo yanayoratbiwa na Taasisi ya Uongozi yana lengo la kuwaongezea ujuzi maafisa hao waaandamizi wa polisi na yatajikita katika maeneo ya muundo wa Jeshi la Polisi, Usalama wa nchi, maadili na rushwa, uongozi na utendaji binafsi, mahusiano yenye tija na akili hisia.

[caption id="attachment_36845" align="aligncenter" width="900"] Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption]

Mkurugenzi Ngimba pia aliwakumbusha makamanda hao wa jeshi hilo kuzingatia maadili na nidhamu kwa sababu ni moja ya nguzo muhimu za utendaji. Aidha, amewaagiza maafisa hao kuakikisha  wanawachukulia hatua stahiki maafisa na maaskari walio chini yao pale wanapojihusisha na vitendo vyenye kulichafua jeshi la Polisi kama vile rushwa na utovu wa nidhamu.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.  Joseph Semboja  amesema kuwa mafunzo hayo  yameandaliwa kwa kushirikina na Jeshi hilo na  kufanyika kwake ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuimarisha utawala bora hapa nchini.

Aliongeza kuwa analipongeza Jeshi hilo kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo yanayolenga kuimarisha utendaji wake.

[caption id="attachment_36846" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya makamanda wa Polisi wakifuatilia mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption]

“Utendaji mzuri wa Jeshi la Polisi unajenga sifa nzuri kwa Serikali kutoka kwa wananchi wanaopata huduma kila siku kwani hili ndilo eneo ambalo taswira ya Serikali inaonekana kwa haraka”. Alisisitiza Prof. Semboja.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Saimon  Siro, Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, Kamishna wa Polisi, Albert Nyamhanga amesema kuwa nchi iko shwari na makosa ya jinai yamepungua kufikia asilimia 13.7 kwa sasa kutokana na utendaji  mzuri na ushirikiano uliopo kati ya Jeshi hilo na wananchi.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kufanya tathmini ya utendaji wa Jeshi hilo kujua llipotoka, lilipo na linapoelekea hali itakayosaidia kuboresha utendaji wake.

Naye Mkuu wa  Mfunzo na Operesheni wa Jeshi hilo, Kamishna wa Polisi, Nsato Marijani ameishukuru Taasisi ya Uongozi kwa kutenga muda na rasilimali fedha kufanikisha mafunzo hayo yanayotarajiwa kuboresha ufanisi kwenye taasisi hiyo muhimu nchini.

[caption id="attachment_36847" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Issa Ngi'mba akiteta jambo na na Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu ya Jeshi la Polisi Kamishna Albert Nyamuhanga wakati wa mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption] [caption id="attachment_36848" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya Makamanda wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo maalum wa Jeshi hilo wakati wa mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption] [caption id="attachment_36851" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu ya Jeshi la Polisi Kamishna Albert Nyamuhanga  akizungumza wakati wa mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption] [caption id="attachment_36849" align="aligncenter" width="900"] Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna mwandamizi wa Jeshi la Polisi Giles Muroto akizungumza wakati wa mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption] [caption id="attachment_36850" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Issa Ngi'mba (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya makamanda wa Polisi wa Mikoa na wale wa Makao makuu ya Jeshi hilo.wakwanza kutoka kulia walioketi ni Mkuu wa Jeshi hilo mstaafu Said Mwema.[/caption]

(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi