Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ulinzi waimarishwa soko la Madini Chunya-DC Mahundi
Dec 04, 2019
Na Msemaji Mkuu

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, MaryPrisca Mahundi amesema ulinzi umeimarishwa katika Soko la Madini Chunya tangu lilipozinduliwa  mnamo tarehe 02 Mei, 2019.
Akizungumza kupitia mahojiano kwa ajili ya maandalizi ya kipindi maalum kuhusu Mafanikio kwenye Sekta ya Madini leo tarehe 04 Desemba, 2019 mjini Chunya mkoani Mbeya amesema kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa soko wafanyabiashara wa madini hawakuwa na uhakika wa usalama wa biashara yao, lakini kwa sasa wanafanya biashara katika mazingira salama na kulipa kodi mbalimbali Serikalini.
Aliongeza kuwa, mbali na uwepo wa ulinzi wa uhakika katika Soko la Madini, Ofisi yake imeimarisha ulinzi katika vituo vya kununulia madini kwa kuweka ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na Kata mblimbali.
Aliendelea kusema kuwa, Ofisi yake imepanga mikakati ya kuimarisha ulinzi katika   Soko la Madini ikiwa ni pamoja na kuweka kamera maalum.
Katika hatua nyingine, Mahundi alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa usimamizi wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, na maboresho ya Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za madini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi