Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Machimbo ya Buhemba Kukamilika Kabla ya Januari 10 Mwakani.
Dec 28, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_25741" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye eneo la machimbo ya Dhahabu la Buhemba. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.[/caption]

Serikali imeagiza kufikia Januari 10, 2018 Ukaguzi wa Usalama kwenye eneo la Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba, Wilayani Butiama Mkoani Mara uwe umekamilika ili shughuli za uchimbaji zilizokuwa zimesimamishwa ziruhusiwe.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi ya machimbo husika pamoja na kuzungumza na wachimbaji waliosimamishwa kuendeleza shughuli zao hadi hapo ukaguzi utakapokamilika.

“Hatuwezi kuufungua mgodi leo hii bila kukamilisha zoezi la ukaguzi kwahiyo kabla ya Tarehe 10 mwezi ujao, Wakaguzi wawe wamekamilisha ili mgodi uanze kazi na shughuli za uchumi zilizokuwa zikifanyika mgodini hapa zirejee,” alisema Nyongo.

[caption id="attachment_25743" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya Wachimbaji kwenye Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba.[/caption] [caption id="attachment_25744" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi wakati wa ziara yake kwenye eneo la machimbo ya dhahabu la Buhemba, Wilayani Butiama, Mkoani Mara.[/caption]

Alisema shughuli hiyo ya ukaguzi inapaswa kukamilika mapema ili maduara yasiyo salama yaweze kutambulika na yazuiwe na yaliyokuwa salama yafahamike na kuendelezwa.

Nyongo alikumbushia agizo alilotoa kwa Wakaguzi wa Migodi Desemba 14, 2017 Mkoani Tabora alipotembelea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua la kukagua hali ya usalama na kuwasaidia Wachimbaji kuepusha ajali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

“Ninawaagiza kwa mara nyingine Wakaguzi wa Migodi kuhakikisha mnatembelea maeneo ya migodi mara kwa mara ili kuepusha ajali,” aliagiza Naibu Waziri.

Aidha, kwa upande mwingine, Naibu Waziri Nyongo amewataka Wachimbaji wa Madini kote nchini kutambua wajibu wao wa kulipa Tozo na Kodi mbalimbali Serikalini kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

[caption id="attachment_25740" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kushoto) akikagua moja ya shimo la dhahabu kwenye machimbo ya Buhemba.[/caption] [caption id="attachment_25742" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wachimbaji kwenye Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).[/caption]

Alisema Serikali haina kikwazo na wachimbaji wadogo na inafanya jitihada za kuwasaidia kuwa na uchimbaji wenye tija hata hivyo alisema wanapaswa kutambua wajibu wao wa kulipa kodi ambayo itawanufaisha wao kama wachimbaji lakini pia Jamii inayozunguka maeneo yenye migodi na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa Rasilimali Madini ni kwa ajili ya Watanzania wote na kwamba kila Mwananchi anayo haki ya kunufaika nayo kwa namna moja ama nyingine mojawapo ikiwa ni manufaa yatokanayo na kodi zinazolipwa kutokana na shughuli za uchimbaji.

Vile vile lengo la Serikali ni kuwarasimisha  Wachimbaji wa Madini kwa kuwapatia Leseni za Uchimbaji ili wachimbe kwa kufuata utaratibu unaotakiwa kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya Mwaka 2017.

Naibu Waziri Nyongo yupo Mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili ya kukagua shughuli za uchimbaji wa madini kwenye maeneo mbalimbali yenye migodi pamoja na kuzungumza na wachimbaji ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi