Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujenzi Mradi Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji Maji Dar Wafikia Asilimia 62
Dec 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24176" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo (kushoto) akimuelezea Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele hatua zilizofikia katika kutekeleza mradi wa uboreshaji usambazaji maji katika jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya mradi huu leo.Kutoka kulia ni Mhandisi Godwini Mlay na Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.[/caption] [caption id="attachment_24177" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele akitoa maelekezo kwa wakandarasi wa mradi wa uboreshaji usambazaji maji katika jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya mradi huo leo.Kutoka kushoto ni Makamu Rais wa Kampuni ya Jain Irrigation System Ltd ambao ndiyo mkandarasi mkuu wa mradi huu Bw. Anil Vitankar, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo na Meneja Mradi wa Kampuni ya Wapcos Ltd Mhandisi P. G. Rajan.[/caption] [caption id="attachment_24178" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo akimuelezea Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele(kushoto)hatua zilizofikia katika kutekeleza mradi wa uboreshaji usambazaji maji katika jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya miradi hiyo leo.Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja na kushoto ni Meneja Mradi wa Kampuni ya Wapcos Ltd Mhandisi P. G. Rajan.[/caption] [caption id="attachment_24179" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wafanyakazi wakitandaza bomba katika eneo la Kibamba kama walivyokutwa wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele (hayupo pichani) kukagua maendeleo ya mradi huo leo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo amefanya ziara na kukagua ujenzi wa matenki tisa katika maeneo ya Mabwepande, Salasala, Makongo/ Changanyikeni, pamoja na ulazaji wa mabomba.[/caption] [caption id="attachment_24180" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji akikagua maungio ya bomba linalotandazwa katika maeneo ya Kibamba alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi uboreshaji usambazaji maji Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_24181" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele (katikati) akipewa maelezo na Meneja Miradi wa Kampuni ya Wapcots Ltd Bw. P. G. Rajan kuhusu ujenzi wa tanki la maji wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi uboreshaji usambazaji maji Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi. Romanus Mwang’ingo.[/caption] [caption id="attachment_24182" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wanajenga mradi uboreshaji usambazaji maji Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huu leo. (Picha na: MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi