Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujenzi wa Miundombinu Watajwa Kuchochea Ukuaji wa Uchumi
Dec 31, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49959" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Serikali katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/20 na hali ya uchumi wa Taifa leo Jijini Dodoma[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Uwekezaji katika sekta za miundombinu umetajwa kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi mijini na vijijini kufikia asilimia 7.0 mwaka 2018.

Akizungumza leo Jijini Dodoma  kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2019 na tathmini ya utekelezaji wa Bajeti kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa sekta zilizokua kwa kasi katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2019 ni pamoja  na ujenzi asilimia 16.5, uchimbaji wa madini na mawe asilimia 13.7,habari na mawasiliano asilimia 10.7, maji asilimia 9.1 na usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 9.0

“Mwaka 2018, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa nchi za SADC, nchi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki na nchi ya tano kwa nchi zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara ikitangulia na Eritrea asilimia 12.2, Rwanda asilimia  8.6, Ethiopia 7.7 na Ivory Cost 7.4”, alisisitiza Dkt. Mpango

[caption id="attachment_49960" align="aligncenter" width="750"] Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Frolens Luoga akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kuhusu utekelezaji wa Bajeti kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2019/20 na hali ya uchumi wa Taifa leo Jijini Dodoma.[/caption]

Akifafanua, Dkt. Mpango amesema kuwa katika kipindi cha Januari hadi June 2019, Pato la Taifa lilikua kwa kasi ya asilimia 6.9 ikilinganishwa na asilimia 6.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Akizungumzia akiba ya fedha za kigeni Dkt. Mpango amesema kuwa inatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa kipindi cha miezi 6.1

“Mwaka 2018, uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.0 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2017 na asilimia 6.9 kwa mwaka 2016”, alisisitiza Dkt. Mpango

[caption id="attachment_49961" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa uchumi kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2019/ 20 na hali ya uchumi wa Taifa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango leo Jijini Dodoma.[/caption]

Akizungumzia ukusanyaji wa mapato Dkt Mpango amesema kuwa mapato yasiyo ya kodi yamefikia bilioni 1,012.8 ikiwa ni asilimia 86.5 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 1,170.3.

Kwa upande wa mapato ya Mamlaka za Serikali za mitaa ni shilingi bilioni 309.4 ikiwa ni asilimia 95.0 ya kukusanya shilingi bilioni 325.6

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa mkutano huo leo Jijini Dodoma

Mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya Serikali za mitaa katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2019, yalifikia shilingi Bilioni 8,501.4 sawa na asilimia 94.4 ya lengo la kukusanya shilingi Bilioni 9,010.2 katika kipindi hicho.

Katika kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo ya utawala wa Mhe. Rais Dkt. Magufuli, Uchumi umekua kwa wastani wa asilimia 6.9.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi