Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wajube wa Kamati za Wilaya wa TSC Watakiwa Kuzingatia Maadili.
Jan 26, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27917" align="aligncenter" width="750"]  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe. Selemani Jafo akifungua Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani  Jafo amewataka Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi wakizingatia sheria na taratibu zinazowasimamia walimu ili kuleta matokeo chanya wakishirikiana na Wajumbe wa Kamati za Wilaya.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku moja kwa wajumbe wa Kamati hizo kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro kilichofanyika leo Mkoani Dodoma, Waziri Jafo amesema kuwa wajumbe hao wana jukumu kubwa la kusimamia masuala ya walimu ikiwemo nidhamu.

[caption id="attachment_27918" align="aligncenter" width="750"] Katibu wa Tume ya Walimu (kushoto aliyesimama) Mwl. Winifrida G. Rutaindurwa akiwasilisha taarifa ya Tume katika Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_27919" align="aligncenter" width="750"]  Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bw.Oliva Paul Mhaiki akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.[/caption]

“Kwa nafasi yangu kama kiongozi wenu, napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha kwamba, moja ya majukumu yenu ni kusimamia ajira na nidhamu kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari Tanzania Bara,” alisisitiza Mhe. Jafo

Amesema kuwa anatambua kazi kubwa inayofanywa na Tume hiyo na Makatibu hao katika ngazi ya Wilaya, hali ambayo imetoa mwelekeo mpya kwa Serikali ambapo itaweka kipaumbele katika kuimarisha na kuijengea uwezo Tume hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Mhe. Jafo amewataka wajumbe wa kamati za Wilaya kuhakikisha kuwa wanashirikiana na waajiri ili walimu wapandishwe vyeo na madaraja kwa wakati kama wanavyostahili kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa.

[caption id="attachment_27920" align="aligncenter" width="750"]  Baadhi ya wajumbe wakifuatilia Mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume  hiyo Oliver Mhaiki amesema kuwa kikao kazi hicho kimewashirikisha wajumbe wa kamati za Tume hiyo ngazi ya Wilaya wapatao 114 kutoka Wilaya 19 za Mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro.

Aliongeza kuwa moja ya majukumu ya Tume hiyo ni kusimamia masuala ya ajira za Walimu ikiwa ni pamoja na kutoa barua za ajira rasmi, kuthibitishwa kazini, kupandishwa vyeo, kubadilisha kazi, kuandaa tange za Wilaya, kupitisha na kuratibu maombi ya kuajiriwa upya kwenye utumishi wa Umma.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bibi Getrude Rutahindurwa amesema kuwa Tume hiyo imetoa uamuzi kwa mashauri ya nidhamu 321 kati ya 1,270 yaliyorithiwa kutoka iliyokuwa Idara ya Utumishi wa Walimu (TSD)  na mashauri 949 yaliyobaki yalirejeshwa Wilayani ili kuhitimishwa kwa sheria mpya.

[caption id="attachment_27921" align="aligncenter" width="750"] Waziri WA Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Aliyekaa katikati) katika Picha ya Pamoja na Sekretariet ya Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.[/caption]

Aliongeza kuwa idadi ya Walimu waliokuwa wamekasimiwa kupanda cheo mwaka 2015/2016 ni 85,945 na kati ya hao, Walimu 38,883 walipandishwa vyeo japo hawajarekebishiwa mishahara ambapo walimu 47,062 wamepandishwa vyeo na kurekebishiwa mishahara.

Aidha Walimu 2,789 walisajiliwa na 2,173 walidhibitishwa kazini, 81 walibadilishiwa kazi baada ya kujiendeleza, walimu wa pesheni 23, mikataba 91 na mirathi 31 walishughulikiwa na hesabu kupekekwa hazina ili walipwe mafao yao.

Tume ya Utumishi wa Walimu ilianzishwa kwa sheria Na.25 ya mwaka 2015 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2016 ambapo Tume hiyo ina Ofisi katika Wilaya 139 Tanzania Bara ikiwa na majukumu ya kumshauri Waziri kuhusu kuboresha utumishi wa Walimu, kusimamia programu za  mafunzo ya walimu kazini, kuhakikisha uwiano sawa katika upangaji wa walimu ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

           

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi