Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Trilioni 3.867 Kuimarisha Ujenzi, Uchukuzi
May 25, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha bajeti ya shilingi trilioni 3.867 ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.

Kwa mujibu wa bajeti hiyo iliyoidhinishwa leo jijini Dodoma, Wizara hiyo inatarajia kutumia jumla ya shilingi trilioni 3.867, kati ya fedha hizo shilingi trilioni 1.466 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na shilingi trilioni 2.401 ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi.

Akiwasilisha bajeti hiyo jana, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema sekta ya ujenzi itatumia shilingi 44.293 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara katika sekta hiyo na taasisi ambapo shilingi 40.639 ni za mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 3.654 ni za matumizi mengineyo.

“Bajeti ya Maendeleo ni Shilingi 1,421,542,185,800.00 ambazo zinajumuisha Shilingi 1,168,576,368,800.00 fedha za ndani na Shilingi 252,965,817,000.00 fedha za nje.

“Fedha za ndani zinajumuisha Shilingi 599,756,467,800.00 za Mfuko wa Barabara na Shilingi 568,819,901,000.00 za Mfuko Mkuu wa Serikali,” amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, sekta ya uchukuzi itatumia shilingi bilioni 94.547 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo shilingi bilioni 67.476 ni za mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 27.071 za matumizi mengineyo.

“Miradi ya Maendeleo imetengewa Shilingi 2,306,234,938,000.00 Kati ya fedha hizo, shilingi 2,192,771,622,000.00 ni fedha za ndani na shilingi 113,463,316,000.00 ni fedha za nje,” ameeleza Waziri Mbarawa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi