[caption id="attachment_43563" align="aligncenter" width="619"] Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Nishati yaomba Kuidhinishiwa Shilingi Trilioni 2.142 ikilinganishwa na shilingi Trilioni 1.692 iliyotengwa kwa mwaka 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 26.6 kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na kuanza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa Rufiji utakaozalisha megawati 2,115 utakapokamilika.
“ Fedha nyingi za ndani za miradi ya maendeleo zilizotengwa kwa mwaka 2019/2020 zimeelekezwa katika miradi mitatu ya kimkakati ambazo ni shilingi trilioni 1.86 sawa na asilimia 95.1 ya bajeti yote ya ndani.” alisisitiza Dkt. Kalemani.
wa Mto Rufiji MW 2,115 uliotengewa shilingi Trilioni 1.44, Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Shilingi Bilioni 363.11 na Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Kinyerezi 1 Extension MW 185 shilingi Bilioni 60. Aliongeza kuwa, Bajeti ya mwaka 2019/2020 inalenga kutekeleza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wenye gharama nafuu. [caption id="attachment_43564" align="aligncenter" width="900"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dastan Kitandula akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo leo Bungeni mara bada ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption]Vilevile, Bajeti hiyo imelenga kuimarisha shughuli za utafutaji na biashara ya mafuta na Gesi asilia pamoja na kuwezesha wananchi kunufaika na rasilimali hizo.
Lengo jingine ni kuwezesha ujenzi wa uchumi wa Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hali itakayosaidia kujenga uchumi jumuishi na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wote hasa wale wanaoishi vijijini.
Akizungumzia upatikanaji wa mafuta hapa nchini Dkt. Kalemani amesema kuwa umeendelea kuimarika kupitia utaratibu wa Serikali kuagiza mafuta kwa pamoja kupitia Wakala wa uagizaji Mafuta kwa pamoja.
“ Kati ya mwezi Januari hadi Desemba, 2018 jumla ya lita Bilioni 5.70 za mafuta ziliagizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara sawa na ongezeko la asilimia 6.3 ikilinganishwa na lita Bilioni 5.36 zilizoagizwa mwaka 2017,” alisisitiza Dkt. Kalemani
[caption id="attachment_43562" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akisistiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya umeme .Kwa upande wa usambazaji wa Gesi asilia Dkt. Kalemani amesema kuwa matarajio ni kuunganisha wateja zaidi ya 500 katika Jiji la Dar es Salaam hali itakayosaidia kupunguza gharama za maisha kwa wananchi wote watakaoungnishiwa huduma hiyo.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika kuunganisha viwanda na huduma ya Gesi asilia amesema kuwa zoezi hilo linaendelea na viwanda kadhaa vimeshaunganishiwa.
Kwa upande wa makisio ya makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2019/2020 yanatarajiwa kuwa shilingi bilioni 602.05 sawa na ongezeko la asilimia 52.6 ikilinganishwa na shilingi Bilioni 394.45 lililokuwa lengo la mwaka 2018/19. Ongezeko la makisio ya makusanyo limetokana na kuongezeka kwa matumizi ya rasilimali Gesi asilia.
[caption id="attachment_43565" align="aligncenter" width="900"] Mbunge wa Muleba Kusini Mhe. Charles Mwijage akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020 leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption]Wizara ya Nishati imeomba kuidhinishiwa Shilingi Trilioni 2.142 na Bunge ikilinganishwa na shilingi Trilioni 1.692 iliyotengwa kwa mwaka 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 26.6 kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
[caption id="attachment_43566" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga nje ya viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43568" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya Wakuu wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi , Watendaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakifuatilia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43569" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa baadhi ya wageni waliofika Bungeni kwa lengo la kujifunza shughuli za Bunge mapema leo.[/caption](Picha na Frank Mvungi)