Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TRA Yasajili Walipa Kodi Milioni 4.6
Sep 06, 2023
TRA Yasajili Walipa Kodi Milioni 4.6
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Chande akizungumza wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Ameir Abdalla Ameir
Na Mwandishi Wetu

Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kupanua wigo wa kodi, ambapo hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesajili jumla ya walipa kodi 4,696, 999, ambao ni sawa na asilimia 16 ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.

Hayo yameelezwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Chande Wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Ameir Abdalla Ameir kuhusu asilimia ya wafanyabiashara ambao hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na Serikali inachukua hatua gani kuwafikia.

Mhe.  Mhe. Chande amesema kuwa idadi ndogo ya usajiliwa walipakodi, ikilinganishwa na fursa ya nguvu kazi iliyopo inatokana na sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi hapa nchini kuendeshwa na sekta isiyo rasmi inayokadiriwa kuajiri takribani watu milioni 27.7.

“Hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kurasimisha sekta rasmi ni pamoja na kampeni ya mlango kwa mlango inayolenga kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wasiotambulika, kutenga na kujenga maeneo maalum ya masoko kwa wafanyabiashara wadogo na kuendelea kutoa elimu na ufafanuzi wa kina kwa wananchi kuhusu masuala ya kodi ili kuhamasisha wananchi kurasimisha biashara na shughuli za kiuchumi kwa hiari,” amesema Mhe. Chande.

Vilevile Serikali imeweka mazingira mazuri yanayorahisha usajili wa biashara kwa wananchi wote, ambapo kazi hiyo inafanywa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Viwanda. Aidha, maeneo yenye fursa nyingi za kibiashara, Serikalu inaweka miundombinu wezeshi yakiwemo masoko na kuweka vituo maalum vya kuhamasisha wafanyabiashara kusajili biashara zao.

Ameendelea kusema kuwa, Serikali kupitia BRELA imetoa elimu kwa wafanyabiashara kusajili biashara zao katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya kijiji mpaka ya kitaifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi